Thursday, February 9, 2012

MKUU WA MKOA WA RUVUMA BWANA SAIDI MWAMBUNGU AKAGUA TIMU YA MBEYA CITY ILIYOTOKA SULUHU NA TIMU YA MLALE JKT KATIKA UWANJA WA MAJIMAJI MJINI SONGEA

 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Mwambungu akisalimiana na wachezaji wa timu ya JKT Mlale uwanja wa majimaji Mjini Songea
 Mkuu huyo wa mkoa wa Ruivuma akisalimiana na timu ya Mbeya City katika uwanja wa majimaji
 Benchi la JKT Mlale
 Akisalimiana na Refarii namba mbili Bi.Agnes Alphonce uwajani hapo baada ya kukagua timu hizo
 akimsalimia mlinda mlango wa timu ya Mbeya City
 Kikosi cha Mbeya City
 Kikosi cha Mlale JKT
 Hatari lango la Mlale JKT
 Mwamuzi wa mezani bwana Yusufu Sekile akimwingiza mchezaji wa Mlale JKT
Hekaheka za mechi hiyo mchezaji wa Mlale JKT anajaribu kupiga chenga mchezaji wa Mbeya City.



Mchezo ambo haukuwavutia wapenzi wengi wa Mjini Songea,ambao ulikuwa hauna kasi kama mchezo wa Jumamosi iliyopita kati ya Majimaji na Mlale JKT,katika kipindi cha kwanza JKT walipotezana kidogo kama hofu Fulani,hofu ambayo ilichukua muda mfupi kisha walijipanga kisawasawa kwa kulisakama lango la Mbeya City bila mafanikio.kwa kukosa magoli ya wazi.
Hali hiyo ilikuwa pia kwa Mbeya City kuchaza mchezo wa kuelewana lakini bahati haikuwa yao,walikosa mabao ya wazi kadhaa,na kuwafanya wapenzi wa timu hiyo kujishika vichwa.Hadi filimbi ya mapumziko walikuwa suluhu.
Katika kipindi cha pili hali ilikuwa kama kipindi cha kwanza ambapo mchezo haukubadilika,ndipoMbeya City walifanya mabadiliko ya kumwingiza mchezaji namba 13 Aruni Mohamed,na Mlale JKT nao walifanya mabadiliko ya ku mwingiza mchezaji namba 5 mgongoni Athoni Malindiza Alisema mwamuzi aliyekuwa kwenye meza Bwana Yusufu Sakile wa Songea.
Mechi hiyo ilichezeshwa na Refarii Hassani Mwichumu Kutoka Dar es Salaam na Msaidi Refarii  namba moja bwanaPatriki Mwanakatwe na msaidi Refarii namba Mbili ni Bi. Agnes Alphonce wote kutoka Dar es Salaam.
Kutokana na mchezo huo Mbeya City wana Point 15 na Mlale JKT point 9 wako mbele ya wenzao timu ya Majimaji ambayo leo imefungwa na timu ya Polisi Iringa goli moja kwa sefuri katika dakika za mwisho na kubakiwa na point 8.


No comments:

Post a Comment