Saturday, February 4, 2012

MICHEZO ! ! ! TIMU YA MAJIMAJI AU WANALIZOMBE WAMETOKA SARE NA WASHIKA BUNDUKI WA MLALE JKT. LEO

 Hicho ni kikosi cha wana- lizombe majimaji wakiwa tayari kupambana na JKT Mlale katika uwanja wa majimaji leo.
 Benchi la tiimu ya Majimaji wa kwanza Kocha wa timu hiyo Mchezaji wa zamani Peter Mhina akiangali timu yake inavyo pambana na washika bunduki hao wa Mlale JKT leo katika pambano la Ligi ya taifa Daraja la kwanza.
 Goli kipa wa JKT Damas Victor Manyika akiokoa mpira wa hatari kipindi cha kwanza katika uwanja wa majimaji leo.
 Kikoai cha Mlale JKT kikiwa fit kwa pambano na Majimaji
Ilikuwa hatari katika lango la JKT mlale katika kipindi cha kwanza.



LIGI ya Taifa Daraja la kwanza iliyoendelea leo katika kiwanja cha majimaji Mjini Songea leo,kati ya timu za Majimaji na Mlale JKT wameshindwa kutambiana mbele ya wapenzi wa timu zote mbili.

 Katika kipindi cha kwanza timu zote mbili zilicheza katika kiwango kinacho fanana,ingwa majimaji walikosa mabao mawili ya wazi,hadi filimbi ikipigwa ya kipindi cha kwanza hakuwepo aliyeona mlango wa mwenzake.

Katika kipindi cha pili JKT walilielemea  sana lango la majimaji lakini  juhudi zao hazikuzaa matunda.wakatoka rezo rezo .na kugawana pointi.

Kwa mujibu wa katibu Mkuu wa Timu ya Majimaji Bwana Henry Kabera,alisema kuwa leo kulikuwa na viwanja vitatu vilivyo endelea na Ligi hiyo alivitaja viwanja hivyo kuwa ni pamoja na Majimaji  Ruvuma,Mbeya na Morogoro.

Kabera alisema Timu za majimaji,JKT na Polisi Iringa wana point 7 kila mmoja Mbeya City ina point 10 ambapo Prison Mbeya ina point 5,kutokana na matokeo ya leo Majimaji itakuwa na point 8 na Mlale JKT pia point 8,

Aidha magoli keepers wa timu zote walikuwa makini katika kulinda milango yao,Bwana Damas David Manyika wa JKT na Rambon Asheri wa timu ya Majimaji walitetea hadi kipenga cha mwisho.

No comments:

Post a Comment