Monday, January 30, 2012

Wazazi kuchangia chakula shule ya sekondari Kalembo WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Kalembo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wanachangia sh. 30,000 kwa muhula kwa ajili ya kupatiwa chakula cha mchana na uji wakati wa asubuhi,ingawa kiasi hicho hakitoshi. Mkuu wa shule ya sekondari Kalembo Bwana Bosco Haule alizungumzia umuhimu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari mkoani hapo na nchi nzima kwa ujumla alipoitembelea ofisi za TUJIFUNZE leo. Bw.Haule alisema kuwa utaratibu wa kutoa chakula katika shule yake haukuanza hivi karibuni,bali ulianza toka mwaka 2005,kwa kutumia Bodi ya shule kuwahamasisha wazazi wenye watoto ambao wanasoma katika shule hiyo kwa kuchangia sh.30,000 kwa muhula. Alisema mchango wa sh.30,000 kwa muhula kwa kipindi hiki akitoshi,lakini kwa kubana matumizi wamefanikiwa kutoa uji na chakula cha mchana ,ambacho ni ugali kwa maharage,ingawa bei ya maharge hayo iko juu ikilinganishwa na bei ya mahindi katika mkoa wa Ruvuma. Kuhusu walimu Bw.Haule alisema walimu nao ili waweze kufanya kazi kwa usahii,na wao wanapata chai na chakula cha mchana kwa kuchangia sh.10,000 kila mmoja. Aidha Mkuu wa Shule huyo alisema kuwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawakuchangia fedha au nafaka kwa ajili ya chakula

Mkuu wa shule ya Kalembo liyoko Matogoro nje kidogo na Manispaa ya Songea Bwana Bosco Haule akielezea jinsi alivyo fanikiwa kuwapa chakula cha mchana wanafunzi wa shule yake.Ansema ili chakula kipatikane shuleni ni vyema kufanya mikutano na wazazi wakubaliane kuchanga fedha na kiasi cha kuchangisha kwa kila mzazi.



WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma katika shule ya sekondari Kalembo Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma wanachangia sh. 30,000 kwa muhula kwa ajili ya kupatiwa chakula cha mchana na uji wakati wa asubuhi,ingawa kiasi hicho hakitoshi.

Mkuu wa shule ya sekondari Kalembo Bwana Bosco Haule alizungumzia umuhimu wa kutoa chakula kwa wanafunzi wanaosoma shule za msingi na sekondari  mkoani hapo na nchi nzima kwa ujumla alipoitembelea ofisi za TUJIFUNZE leo.
Bw.Haule alisema kuwa utaratibu wa kutoa chakula katika shule yake haukuanza hivi karibuni,bali ulianza toka mwaka 2005,kwa kutumia Bodi ya shule kuwahamasisha  wazazi wenye watoto ambao wanasoma katika shule hiyo kwa kuchangia sh.30,000 kwa muhula.
Alisema mchango wa sh.30,000 kwa muhula kwa kipindi hiki akitoshi,lakini kwa kubana matumizi wamefanikiwa kutoa uji na chakula cha mchana ,ambacho ni ugali kwa maharage,ingawa bei ya maharge hayo iko juu ikilinganishwa na bei ya mahindi katika mkoa wa Ruvuma.
Kuhusu walimu Bw.Haule alisema walimu nao ili waweze kufanya kazi kwa usahii,na wao wanapata chai na chakula cha mchana kwa kuchangia sh.10,000 kila mmoja.
Aidha Mkuu wa Shule huyo alisema kuwa kwa wanafunzi ambao wazazi wao hawakuchangia fedha au nafaka kwa ajili ya chakula cha watoto wao,hawapati chakula,ili wazazi wenye watoto hao waone umuhimu wa kupata chakula kwa wanafunzi.Nakwamba kila mwanafunzi anatumia sh.350/=  kwa siku.

No comments:

Post a Comment