Wednesday, January 11, 2012

MUHULA WA MASOMO KWA SHULE ZA MSINGI UMENZA JUMATATU WIKI HII KATIKA SHULE YA MSINGI USAGARA KIMAMBA KILOSA WANAFUNZI WANAONEKANA WENYE FURAHA

 Ni saa moja na nusu asubuhi ya Jumatatu wiki hii wanafunzi wa shule ya msingi Usagara Kimamba Kilosa Mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye sare zao za shule kutoka awali wenye sare za kijani hadi darasa la saba wakiimba wimbo wa Taifa na wimbo wa shule ,wakiwa na walimu wao wakiwa na ari ya kuanza ngwe ya kwanza ya kazi yao ya kuelimisha Taifa hili.
 Wanafunzi wa Awali wakiwa na kaka na dada zao kwenye mistari ,tayari kwa kuingia madarasani.
 Hao ni wanafunzi wa darasa la saba ambao wanaingia darasa hilo kwa mara ya kwanza kutoka darasa la sita.
 Baadhi ya walimu wa shule hiyo waliyo kutwa na blog hii asubuhi hiyo wakiwa wakisubiri wanafunzi kuingia madarasani ili wakafanye kazi yao ya kufundisha.Ambapo hapo awali kazi hii nyeti ilikuwa ni kazi ya wito,bali sasa imekuwa ni kazi kama kazi nyingine,wanaingia hata wale wasiyo na wito kwa kuwa walikosa kazi.walimu kama hao wanakosa maadili ya ualimu.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba waliyokuwa wakifanya usafi kwenye ofisi ya mwalimu mkuu wakijisifia kuwa waote watafaulu mtihani,shule hiyo ina wanafunzi 65 wa Awali na 540 wa shule ya msingi na kufanya idadi ya wanafunzi 605.

No comments:

Post a Comment