Wednesday, January 11, 2012

kilio cha wakulima wa Wilaya ya Kilosa,kinagonga mwamba kila mara kwa uongozi wa Wilaya hiyo wanapopeleka kesi za kuliwa mazao yao na ng'ombe wa wafugaji wa kimasai

 Makundi kwa makundi ya ng'ombe wa wafugaji wa kabila la wamasia yamekuwa kero na hasara kubwa kwa wakulima wa wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro.
Wakulima wa Tarafa ya Kimamba,Madoto,Rudewa Msowero, wanapata shida sana na wafugaji hao ambao wanalisha ngombe wao kwenye mashamba ya watu kwa makusudi.'mashamba tuna kodishwa kwakuwa maneo tunayolima na mashamba ya mkonge ya mwei wa kukezaji,wakati  mazoa yakikomaa wamasai wanaingiza ng'ombe zao kulisha,ukipeleka kesi hiyo kwenye uongozi wa wilaya wanakuambia nenda tunashughulikia,utapigwa kalenda,kwa kuwa wamasai hao wana fedha za kutoa kwa wakubwa na wakulima hatuna kitu.' walisema wakulima hao ambao hawakupende majina yao yajulikane.na kwamba walisema viongozi wa ngazi zote wananufaika na kuliwa kwa mazao ya wakulima ktika wilaya hiyo.
Jeuri ya fedha inawapa kichwa maji wamasai wafugaji,wakulima walala hoi wanambulia patupu,Ukweli Serikali ijaribu kuangalia hakiza wa wakulima hao,bila ubaguzi wa nani ana fedha na mwengine hana basi akose haki yake,ndiyo kila mika kuna kuwa na mapigano kati ya wakulima na wafugaji hao katika wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment