Friday, January 27, 2012

USEMI WA BONGO NIMEUSHUHUDIA LEO HAPA JIJINI DAR ES SALAAM

 Mpiga picha wa Blog hii leo alipata nafasi ya kuona jinsi wabongo wanavyo jishughulisha na maisha,hapo ni eneo la Feri Jijini Dar es salaam maarufu kwa uzaji wa samaki wabichi pia wanaokaangwa.wakazi  wengi wanatoka kila pembe ya Jiji hilo kufika hapo kwenda kununua samaki wa kwenda kuwauza baada ya kuwakaanga,wasomesha watoto wao,wanajenga,aidha mahitaji yo yote muhimu wanapata kutokana na shughuli hizo,' Hiyo ndiyo bongo'
 Pilika pilika foleni ya magari ni kitu cha kawaida hasa muda wa asubuhi watu wanakwenda kazini na muda wa kurudi kazini.Hapo ni maeneo ya Manzese  Dar es salaam.
 Wanafunzi wasukuma mikokoteni ya kuuzia maji nao wako katika harakati ili mradi wawahi kwenye maeneo husika.Mpiga picha aliwakuta hao maeneo ya Mabibo Jijini Dar es salaam Leo.
Wenye baiskeli na watembea kwa mguu katika Jiji hilo ni wengi kushinda wanaokuwa kwenye usafiri,Lakini yote ni mema Jiji au mji hauwezi kuwa na sifa kama watu wa ina na nafasi tofauti watakosekana wote kwa pamoja ndiyo wanaofanya Jiji liitwe hivyo.


JIJI la Dar es Salaam wameliita bongo kutokana na watu wa Jiji hilo hutumia akili sana ili waweze kuishi katika Jiji hilo liitwalo Dar es Salaam,maana si dhani watu hao wana lala saa ngapi maana magari usiku kucha yanapita kuelekea yaendako  na yale yatokako.Mkazi mmoja hakupenda jina lake lijulikane maeeneo ya Feri ambako asilimia kubwa ya wakazi wa Jiji  Hilo ndipo wanapo patia maisha yao,alisema .
‘ Saa  kumi ya usiku kuna baadhi ya wafanyakazi wanaamka kujiandaa kwenda kwenye vituo vya daladala,na wengine wanajiandaa kuja hapa Feri kuwasubiri wavuvi kutoka kuvua samaki ili wanunue waende kuwakaanga na kuwauza,na asilimia kubwa ni akina mama.’
Lazima kutumia akili,kwenye uzalishaji mali ujasiliamali mdogomdogo,biashara za kuuza maji,matunda,mboga,Juisi,vyakula,plastiki za maji vyuma chakavu mama na baba ntilie.
Pia wapiga debe,waombaji,matapeli wanaotumia bongo zao kujifanya maofisa wa serikali au shirika Fulani,wanaojifanya wanauza simu ama saa za bei mbaya ,ambao wamewaliza wasafiri wengi Stendi kuu ya  mabasi yendeyo mikoani .Ubungo kwa kuwauzia vipande vya sabuni ama kibao wamevifunga  kwa ustadi kwenye bahasha ya kaki na kumkabidhi msafiri kwenye basi anapo fungua anakuta sabuni au kibao basi,Jamaa anatokomea mkwenye mabasi.hiyo ndiyo bongo.
Kwa utaratibu huo wasafiri wanatakiwa wawe macho,simu na saa mbona zimejaa madukani siku hizi! Kwa nini unataka ‘short cut’waogopeni sana watu hao sanacho kuonyesha sicho atakacho kukukabidhi baada ya kumpa fedha hata angevaa na kuwa nadhifu kiasi gani Wabongo hao.Samahani sio samaki mmoja akioza ndiyo wote hapana ila baadhi ya Wa – Bongo ni wajanja.  

No comments:

Post a Comment