Wednesday, January 11, 2012

SERIKALI IJARIBU KUIOKOA RELI YA KATI ,HALIYA RELI HIYO INASIKITISHA,TRAIN KUPITA KWENYE RELI ILIYO GUBIKWA NA NYASI NI HATARI ,HAKUNA USALAMA

Hiyo ni reli ya kati katika station ya Kimamba Kilosa Mkoa wa Morogoro,hali kama hiyo hapo ni station je katikati ya mikoa ya Dodoma,Tabora,Kigoma,shinyanga na Mwanza hali iko vipi.,Kama mwekezaji yupo basi ifanye jitihada ya kuwarudisha wafanya kazi wa magenge mabo mwanzo walikuwa wanaita pigilia,amabo walikuwa wakifanya usafi katika reli hiyo na wakaguzi wa reli,ili kuwe na usalama wa train. lakini sasa hawapo hao,kwa utaratibu huo ajali zitakosekana?
Reli ya kati ni muhimu sana kwa kusafirisha mizigo kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma,Mwanza na kurudisha mizigo mingine,aidha ilisaidia sana wasafiri amabo hawana kipato cha kutosha ,hasa nauli za mabasi,Hebu serikali hasa wizara ya miundo mbinu ijariku kulikwamua shirika hilo kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment