Sintosahau siku ambayo Mke wangu na mjukuu wangu Sara na mama mkwe Coleta ambayo wangepoteza maisha yao kwa kifo kibaya cha moto,ukliyotokea tarehe 28/12/2011 saa 1.30 usiku,moto uliyoanzia sitting room na dining room wakati Mrs Sikapundwa akiwa ndani na watoto wakiwa chumba kingine,ambapo mama huyo aliskia mlio kama bom,kumbe zilikuwa TV vikipasuka ndipo alipo gundua kuwa hatari.Mama ni yule mwenye nguo nyeupe na Sarah ni yule aliyeshika kiuno.
Nilikuwa nashangaa jinsi moto ulivyo tekekteza mlango na dirisha.ama kweli kama siku za kufa mtu bado ,chuki na hila za binadamu haziwezi kufua dafu.Lakini watu husema kwa nini kumwingilia Mungu kazi yake?,kazi ya kuua ni ya Mungu peke yake,wengine wanamwingila.
Ukianagalia miujiza ya Mungu ,huwezi amini,kwenye ngzi ndogo kuna dirisha la blue,basi kwenye dirisha lile ndipo Mke wangu Mrs E.Sikapundwa alipovutwa na watu waliyofika kwenye tukio hilo siku hiyo ambayo shetani alitawala katika nyumba ile,lakini Mungu alikataa.
Nawashukuru majirani,Kikosi cha kuzima moto cha Manispaa ya Dodoma,Walimu wa shule za msingi za manispaa hiyo hususani shule ya msingi Makole ambapo mama huyo anafundisha hapo,Jumuiya tunayosali ya Makole na watu wote waliyoziokoa roho za wanafamilia yangu.sina cha kuwalipa bali na sema asante,
No comments:
Post a Comment