Tuesday, February 28, 2012

KUMBUKUMBU ZA MASHUJAA WA KINGONI YALIHAMASIHWA NA UTAMADUNI KAMA HUO

 Kijana Athuman Kenezi alikuwa akicheza ngoma ya kitamaduni,ambapo alivaa mavazi yanayoendana na utamaduni wa mwafrika.Isitoshe alicheza na moto,alikula bila ya kuungua mdomo wake.
i
 Bwana Kenezi akinengua,alijipatia kiasi cha fedha Mkuu wa Mkoa Mhe. Mwambungu ,katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi na wageni wengine walimzawadia kwa uchezaji wake.
 Kama unavyoona wandishi wa habari wapigapicha walivyokuwa wakipata picha alipokuwa meza kuu.
 Hiyo tu haitoshi wazee wa Kingoni na ngoma yao ya Ligiu yenye asili ya Zulu Afrika Kusini nao walitumbuiza.
 Pamoja na Yote palikuwa na tiba mbadala dawa za asili pia zilionyeshwa.
 Kioda nacho kilikuwepo katika kutumbuiza sherehe hizo sambasamba na ngoma ya Beta.
Ngoma ya Beta kutoka Lizaboni Manispaa ya Songea iliyoongozwa na mzee Masetus Ponera ,Angelika Gama katibu Mwenyekiti Alana Nditi kikundi cha wachezaji 15.

WAZEE WA KINGONI WALINYONGWA KWA KUTUMIA KAMBA NA KUZIKWA KATIKA KABURI MOJA WATU 66

 Hapo ni wapigania uhuru waliokataa kutawaliwa na wajerumani walinyongwa kwa kamba hadi kifo.
 katika eneo hilo sasa pamejengwa mnara wa kumbukumbu ambapo katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi. Maimuna Tarishi anaweka silaha Kibonga ama kirungu.
 Kisha walizikwa katika kaburi moja watu 66 ambapo baada ya kuweka mashada ya maua viongozi wa madhehebu ya dini waomba dua zao.

 Shekhe Abdalah Hassan Amiri Mkonyogole wa Msikiti wa Hudda Shehke mkuu wa Mkoa akisoma dua katika kaburi hilo.


Padre Dkt Dunstan Mbano akiendesha ibada fupi ya kuwaombea marehemu hao wakae mahali pema peponi.

TAMASHA LA MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI JANA YAMENDA SAMBAMBA NA KUMUENZI DKT RAURENCE MTAZAMA GAMA

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi.Maimuna Tarishi ,alisema  tamasha la makumbusho ya Taifa ya Majimaji yanakwenda sambamba na kumuenzi Dkt Raurence Mtazama Gama kwa mambo mengi ya maendeleo aliyoyafanya enzi ya uhai wake.Alisema Dkt Gama atakumbukwa kwa mambo mengi yakiwemo Uwanja wa michezo wa Ally Hasani Mwinyi Tabora,majimaji na zimani moto Songea..
 Aidha alisema masuala ya utalii yalikuwa mikoa ya kaskazini na Magharibi,lakini sasa Makumbusho ya kusini yatakuwa ni kivutio kikubwa cha utalii wa utamaduni.
Alisema tangu makumbusho ya majimaji yawe makumbusho ya taifa wageni wengi wandani na nje wametembelea katika makumbusho hayo. kutoka watalii 48 mwaka 2006/7 hadi 1,444.mwaka 2011.na kwamba Bodi ya makumbusho itaendele kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuboresha vivutio vya kitalii katika kanda ya kusini.
 Wazee wa mila wa kingoni wameketi kwenye nyumba ambayo kumehifadhiwa vitu alivyokuwa akitumia Dkt Raurence Mtazama Gama.watalii wanafika kuona baadhi ya zana ambazo alitumia katika uhai wake,na ndiyo mwanzilishi wa makumbusho hayo.
 Kushoto ni mkuu wa wilaya ya Songea Bwana Ole Thomas Sabaya,wakatikati ni Chief wa Kingoni Emannuel Gama na Kulia na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu wakielekea  makumbusho ya majmaji mashuja Mahenge Katika Manispaa ya Songea.
Wanaingia katika maeneo ya mashujaa
 Katibu mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Bi Maimuna Tarishi akiwa katikati ya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mwambungu kushoto na Chief wa wangoni Emannuel Gama kulia wakiwa maeneo waliponyongwa wapigania uhuru wakati wa vita vya majimaji
 Wazee wa kingoni wakionyesha jinsi walivyo weza kupambana na wakoloni wa kijerumani kwa kutumia silaha zao za jadi katika viwanja vya mashujaa wa majimaji.

Wangoni hao na silaha zao za kijadi,ambazo hutumiwa kama ngoma ya Ligiu.yenye asili ya Afrika Kusini ambako walikimbia utawala wa Chaka Zulu.Hata hawa wanaimba nyimbo za kizulu.

Sunday, February 26, 2012

MATUKIO WIKI ILIYO PITA KATIKA MANISPAA YA SONGEA KAMA HIVI ! !

 Askari polisi akionyesha karatasi yenye maandishi ya kiarabu ya tuhumiwa kwa waandishi wa habari katika Hospitali ya mkoa Songea  siku ya vurugu ya maandamano ya kupinga mauaji,baada ya kuwasachi watuhumiwa na kukutwa na hirizi ambayo kwa imani yao ilikuwa ikiwasaidia katika kifanya mauaji na maovu mengine bila kutiwa mbaroni lakini za mwizi ni arobaini.
 Gari la Polisi ambalo lilikuwa likitumika katika kutuliza maandamano siku hiyo ya machafuko katika manispaa ya songea Mkoani Ruvuma.kwa piga risasi hewani na kutupa mabomu ya machozi.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabit Mwambungu akilikuwa akiongea na Kamati ya ulinzi na   usalama ya mkoa na wilaya na viongozi wa serikali wa mkoa na wilaya wakiwemo maafisa Tarafa,watendaji wa kata,Vijiji na mitaa siku ya vurugu hiyo kwa lengo la kurudisha amani iliyokuwepo hapo awali.
 Baada ya tukio hilo Mkuu wa Mkoa alitoa taarifa kwa vyombo vya habari na kutoa taarifa kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuwa wawe watulivu,wasubiri serikali ifanye kazi yake ya kuwasaka wahalifu kwa kushirikiana na wananchi wenyewe pamoja na polisi.
Baadhi ya wananchi katika Stendi kuu ya Songea siku ya maandamano hayo wakati hali hajawa tete sana na mabomu yalikuwa bado kutupwa mfululizao,maana baada ya masaa manne yaliyo fuata hapakuwepo mtu alionekana katika maeneo hayo.
 Mkuu wa mkoa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake siku hiyo isiyo sahaulika na wakazi wa Manispaa hiyo.
 Bwana Fili Karashani wa kwanza aliyesimama kulia,akiongea na waandishi wa habari wa Chama cha Waandishi wa Habari Ruvuma Press Club  katika ukumbi wa SACCOS ya walimu Majengo siku ya kwanza ya mafunzo ya habari za uchunguzi,na ndiyo ilikuwa siku ya vurugu hizo hivyo Bw.Karashani aliwaambia waandishi hao kwenda kwenye matukio na kisha warudi na habari za vurugu hizo ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo siku hiyo.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa na wilaya siku ya machafuko hayo wakiwa katika ukumbi wa Songea Club na viongozi wengine wa mkoa na wilaya na watendaji wa vijiji,kata na mitaa kwa ajili ya kuleta amani.

JUMAPILI YA KWANZA YA KWARESMA ,NI KIPINDI CHA MAJUTO ,KUJICHUNGUZA KATIKA DHAMIRA ZA WA KRISTO WA ROMAN CATHOLIC DUNIANI NAWATAKIA MFUNGO MWEMA

 Waumini wa Roman Catholic katika kanisa kuu la jmbo la Songea wakienda kupaka majivu Jumatano ya majivu ni ishara kuwa ni siku ya waumini hao kuanza mwezi wa toba na mfungo.Ambapo leo ni Jumapili ya kwanza ya Kwaresma Ibada iliyo adhimishwa kwenye makanisa ya RC Duniani kote.
 Askofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Norbert Mtega aliwasihi waumini wake kuwa na toba ya kweli,na wala siyo kujionyesha kuwa unafunga,ni siri ya yule anaye funga na Mungu wake.Na kwamba amaomba amani hasa kipindi cha vurugu zilizotokea Katika manispaa ya Songea zilizosababishwa na maandamano ya kupinga mauaji.
Kila muumini wa dhehebu hilo hupakwa majivu kichwani kwa alama ya msalaba, ambao Yesu kristo alipigiliwa misumari mikono yake na miguuni.kama unavyo muona huyo muumini aliyekwisha pakwa majivu kichani.

Friday, February 24, 2012

WAENDESHA PIKIPIKI KATIKA MANISPAA YA SONGEA SASA KUVAA SARE

 Madereve wa yeboyebo kabla ya kuongea na mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bwana Said Thabit Mwambungu kwenye ukumbi wa Songea Club.
 Baadhi ya viongozu ,wamiliki na waendesha pikipiki katika ukumbi wa Songea Club wakimsubili mkuu wa mkoa mjini Songea.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabit Mwambungu akiongea na madereva wa yeboyebo na wamiliki wa yeboyebo hizo katika ukumbi wa Songea Club jana.
 Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Ole Thomas Sabaya  kisisitiza umuhimu wa kuwa na sare wakati wa kuendesha yeboyebo hizo.
Bw.Mwambungu akishikana mikono na madereva hao baada ya kikao Songea Club jana.



Madereva wa Yebo yebo Songea waandaliwa sare

  • Zenye namba na sehemu anakotoka
  • Ziweze kumtambulisha kiurahisi

MADEREVA yeboyebo katika Manispaa ya Songea wanaandaliwa sare ambazo zitasaidia kumtambua mwendesha pikipiki kuwa ni wa eneo gain,endapo akapatwa na matatizo na mteja wake itakuwa ni rahisi kufuatilia.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma alisema hayo katika ukumbi wa Songea Club jan alipokuwa akizungumza na wamiliki na waendesha pikipiki wa mjini Songea,ambao hawakuweza kufika wote kwenye mkutano huo baada ya wengine kwenda Litola kumzika mwendesha pikipiki mwenzao.
Aidha Bw.Mwambungu aliwaomba waendesha pikipiki hao kuwa makini wakati wa chukua abiria wao kwakuwa abiria wengine si wazuri kwa uhai wao,na kwamba  kazi yao nzuri lakini ikawa mbaya   katika maisha yao kutokana na abiria wanaowachukua hasa ikiwa zaidi ya mmoja.
Alisema kuwa waachane na ushabiki ambao unaweza  ukaleta madhara makubwa katika Jamii kama ilivyo jitokeza katika maandamano waliyoyafanya kwa kuwatupia mawe polisi,ofisi ya CCM mkoa na wilaya,mkuu wa mkoa,Ikulu ndogo na Songea Club kuliko sababisha Jeshi Polisi  jibu kwa piga mabomu ya machozi na silaha za moto.

Kamishina wa Jeshi la Polisi nchini Paulo Chagonji ameongea na waandishi wa habari wa Press club kuhusu ufafanuzi wa vifo vilivyotokea Songea


 Amesema katika vifo vyote vilivyotokea Songea hakuna kilicho husiana na ushirikina,na hakuna hata mmoja aliyetolewa sehemu zake za siri kama ilivyo ripotiwa.aidha alisema katika watu waliyokufa wakati wa kuzuia maandamano ni watu wawili tu ndiyo waliuawa na mmoja alikufa kutokana na ajali ya pikipiki.Alisema na Polisi wote waliyo sababisha mauaji wamechukuliwa hatua za kinidhamu.Na watu waliysababisha vurugu za kupiga mawe ofisi nao wamechukuliwa hatua.
Kamishina ameongea na wanachama wa Press Club leo katika ukumbi wa SACCOS Majengo  katika Manispaa ya Songea  Ruvuma





Wednesday, February 22, 2012

SIJAWAHI KUSHUHUDIA MABOMU YA MACHOZI YANAVYO WASHA MACHONI LAKINI LEO NIMESHUHUDIA,POLISI WALIPO KUWA WAKIRUSHA MABOMU HAYO LEO SONGEA MJINI

Hilo ni moja ya gari la polisi ambalo lilikuwa likigawa mabomu kwa wananchi walioandamani kupinga vifo vya watu vilivyotokea katika Manispaa ya Songea,Lizaboni juzi,Ruvuma jana na Mjimwema leo.
 Vijana hao wenye yeboyebo ndiyo waliyoanzisha  zali hilo baada ya mwendesha yebo mwenzao kuuliwa leo na kutupwa kwenye mto wa Matarawe.
 Wananchi waliyo fukuzwa kutoka stendi kuu ya mabasi wakiwa barabarani,lakini polisi kila walipokuta mkusanyiko waligawa mabomu hayo,inaelekea yalikuwa mengi na hayajatumika,na askari nao toka watoke kwenye mafunzo walikuwa hawajapata kashikashi kama ya leo.Ambapo katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamepata majeraha mbalimbali sehemu zao za mwili.
 Hao ndiyo yebo yebo,hali tete katika Manispaa ya Songea imeonysha wananchi kuwa serikali ipo,na serikali nayo imetambua kuwa wananchi wakuchoka wanafanya matukio yasio na msingi kama hawatekelezewi kero zao.
Hili ni eneo maarufu sana katika Manispaa ya Songea kwa uuzaji wa mitumba,Majengo mabapo huwa watu wanajaa wateja na wauzaji wa nguo hizo,lakini leo hali ndiyo hiyo,kweupe kutokana na polisi.Shughuli zote za uzalishaji mali hazikufanyika kuanzia asubuhi hadi jioni.

Jamani amani bado inatakiwa Tanzania sijui wale wenzetu kila siku wanakimbia wanaisha vipi,sisi tulikuwa kwenye chumba cha mikutano lakini bomu la machozi lilitupwa nje bila sisi kujua,kilichotokea wote tulilia tukawahi kwenda kunawa maji.
Bunduki haina urafiki,ukimwona hata rafiki yako ameishika na kukulenga ujue uko katikati ,ya dunia na mbingu.Hadi hali inatulia mji mzima unanuka mabomu.

LEO SIKU YA MAJIVU DUNIANI KOTE KWA WAUMINI WA ROMAN CATHOLIC,ASKOFU MKUU WA JIMBO LA SONGEA NORBET MTEGA AMEOMBA AMANI ITAWALE

 Askofu wa jimbo kuu la Songea Norbert Mtega akigawa majivu baada ya kuyabariki ili kupaka waumini kichwani kama ishara kuwa binadamu ni mavumbi siku moja atarudi tena kua mavumbi.Ikiwa ni siku ya Jumatano ya majivu,ni kipindi cha mfungo kwa Resma kufanya malipizi ya kutubu dhambi na kujisahihisha pale tulipomkosea Mungu.
 Mhasham  Norbert Mtega akibariki majivu katika ibada ya kupaka majivu katika kanisa la Mtakatifu Matias Mlumba Kalemba mjini Songea leo.
 Askofu Mtega anapakwa majivu na Naibu Askofu
 Askofu Norbert Mtega akiwa na majivu kwenda kuanza kupaka waumini baada ya kumpaka mmoja wa Mapadre wake.Katika mahubiri yake alisema kuwa ni kipindi cha toba,katika roho,watoto,vijana,watu wazima na wazee wafanye toba.
Aidha ametoa wito kwa vijana wa Songea na Nchi nzima kuwa wawe watulivu kunapotokea matukio mabaya,na kwamba wasishindane na vyombo vya dola katika kuchukua sheria mkononi.Pia ameomba serikali kuchukua hatua za haraka pale panapotokea tatizo ,na kwamba kuchelewa kutatua matatizo yanapotokea kwa wananchi kunaleta madhara makubwa.
Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 20 aliyoishi Songea alikuwa hajawahi kuona matukio kama yaliyotokea leo la mapambano kati ya polisi na wananchi mabomu ya machozi na mawe kutoka kwa wananchi.Baba Mtega ameomba ushirikiano wa uongozi wa mkoa na taifa na wananchi ili kuleta amani.

 Waumini wanapaka majivu,Juma tano ya majivu leo katika kanisa kuu la Songea
Waumini wa Roman Catholic Songea wameungana na Waumini wengine duniani katika ibada ya majivu,ikiwa ni mwanzo wa mfungo wa Kwaresma.