Watu wanne watafikishwa mahakamani kesho kufuatia kuibiwa vocha za pembejeo 4,599 zenye thamani ya shilingi 21,114,000.Pembejeo amazo zilitakiwa kupelekwa katika kata 21 lakini kati ya kata hizo kata 9 zimekosa vocha hizo.
Watakao pelekwa mahakamani kesho ni pamoja na Afisa kilimo na mifugo wa Manispaa ya Songea Dkt Frenk Nkoma ,Michaela matembo Mratibu wa Pembejeo wa Manispaa ya Songea,Dani Kagema Mhasibu msaidizi wa Halmashauri hiyo na wakala wa pembejeo Bwana Prosper Mahai.
Inadaiwa kwa katika Kata ya Subira,zilitakiwa kupelekwa vocha 174 lakini hazikupelekwa,Kata ya Lilambo zilitakiwa kupelekwa vocha 120 lakini zimepelekwa vocha 30 tu,Kata ya Lugagala zilitakiwa kupelekwa vocha 100 lakini zimepelkwa 50 tu..
Nyingine ni kata ya kilagano zilitakiwa kupelekwa vocha 130 lakini zimepelekwa vocha 30 tu,na Mlete palitakiwa kupelekwa vocha 122 lakini vocha zilizofikishwa katani hapo ni 50,kufuatia kubainika kwa mgao huo wa vocha hizo polisi wanafuatilia mgawanyo huo.
'Wananchi wa Songea na Mkoa mzima ambao ni wakulima wanaopata shida ya pembejeo kilio chao kimesikilizwa na Mungu; alisema mkulima mmoja ambaye hakutaka ajulikane katika Blog hii.
No comments:
Post a Comment