Huruma imetoweka miongoni mwa watu katika jamii,hayo yamesemwa leo katika mahubiri yake Rv Father Deogratias Nditi katika kanisa dogo kigango cha Matarawe Katika manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.
Father Nditi alisema kwa jamii imekosa huruma,ndiyo maana hawaoneani huruma.Alisema mwaka huu matokeo ya kidato cha nne si mazuri katika Sekondari za kata,si kwa sababu shule hazina walimu wa kutosha na matatizo mengi,si hivyo tu bali kuna watoto wengine wamekosa vitabu,sare.chakula cha kutosha,huwenda hawana wazazi.au wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.Lakini watu wasio na huruma kwa watoto hawa wameshindwa kuwasaidia.hata mtu angetoa daftari tu lingemsadia,ili kupunguza wimbi la vijana wanaoshindwa mitihani yao na kuwa vibaka,na majambazi kwa kukosa kazi hapo baadaye.
Kwaya ya Shirika la Kipapa likiimba wakati wa Ibada iliyoendeshwa na Padre Nditi katika kigango cha Matarawe leo,wakiwemo na viongozi wao walio wachagua kwa kufuata Demokrasia.
No comments:
Post a Comment