Wednesday, January 19, 2011

KILIMO KWANZA HAKITAFANIKIWA KWA KUTOA MFUKO MMOJA KWA MKULIMA


KILIMO kwanza hakitaweza kumnufaisha mkulima iwapo serikali itaendela kumpa mkulima mfuko mmoja wa mbolea ya UREA kwa heka moja ya mahidi kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma.

Wkala wa usambazaji wa pembejeo za kilimo katika Wilaya ya Songea Vijijini na baadhi ya Halmashauri ya Manispaa ya Songea Bi.Matilda Mwenda alisema hayo alipokuwa akihojiwa katika ofisi ya Blog hii leo.

Alisema serikali inatoa ruzuku ya mfuko mmoja wa UREA kwa heka moja kwa mkulima,kitu ambacho kiutaalamu hakiwezi kuleta maendeleo katika KILIMO KWANZA.

Alisema ili lengo la KILIMO KWANZA lifanikiwe,basi serikali itoe mifuko mitatu kwa heka moja kwa kila mkulima ili mazao yapatikane kwa uhakika.

Bi.Mwenda anasamabaza mbolea Madaba,Mshangano,Chandarua,Jeshini Ruhuwiko,Namanyigu na baadhi ya mitaa ya Manispaa ya Songea.

Aidha anawauzia wakulima mbolea ya UREA shilingi 20,000 kwa mfuko na serikali inachangia shilingi 22,000 na kufanya bei ya shilingi 42,000 kwa mfuko mmoja wa mbolea hiyo.

Mbolea nyingine ni CAN shilingi 40,000 kwa mfuko mmoja na SA shilingi 35,000 kwa mfuko.ambapo serikali haitoi ruzuku kwa mbolea hizo  kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment