Friday, January 28, 2011

IJUMAA YA LEO KARIBU KUSINI UKUTANE NA WAGENI KUTOKA WILAYA YA MBINGA MKOA WA RUVUMA

 Wageni wetu waliotutembelea katika ofisi yetu ya TUJIFUNZE KUSINI wakiwa walimu wa Sule ya Sekondari Makita Mbinga Mwalimu Atarasila B.Hyera anayeonyeshwa Gazeti la Tujifunze lililochapwa kwa rangi,na anaye fuatia ni mwalimu Euristar A.Ndunguru wakiwa katika ya Ofisi ya Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE ,pia ni mwenye kiti wa Ruvuma Press Club Bwana Juma Nyumayo anaye onyesha Gazeti na mwenye suti ni Afisa Uzalishaji wa TUJIFUNZE Bwana Joram Mwaipopo.
 Hapa Bwana Juma Nyumayo  karibu na mashine akiwaonyesha wageni wake mtambo wa kuchapia gazeti la TUJIFUNZE na Jarida la Elimu (  Ed- SDP News Letter )
Wilaya ya Mbinga na mwambao wa Ziwa nyasa ambayo sasa ni wilaya mpya,kuna makabila ya Wamatengo,Wamanda,Wanyasa.wana ngoma maarufu sana kama Mhambo unayoiona wakicheza,hiyo ni ya wamatengo,kuna kioda kinachezwa na akina mama wa kimatengo Kimanda,pia kuna Mganda unaochezwa na Wanyasa na Wamatengo ili zimetofautiana katika uchezwaji wake.

1 comment:

  1. Shukrani sana kwa kazi kubwa unayofanya ya kuendesha blogu hii. Mimi huku ughaibuni najisikia vizuri sana kila siku kwa kupata habari na picha unazoleta. Na sio mimi peke yangu. Habari za kwetu Mbinga zinanigusa kwa namna ya pekee, na ndio faida ya mtandao. Endelea kukaza buti, na Mungu akubariki.

    ReplyDelete