Mheshimiwa Diwani wa kata ya chemchem Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Charles Mhagama mwenye suluali ya rangi ya udongo akitoa maoni yake kuhusu Katiba ya Jamhuuri ya muungano wa Tanzania kwa Mwenye kiti wa waandhishi wa Habari Ruvuma Bwana Juma Nyumayo aliyevaa shati mikono mifupi Mateka leo.
Mhe.Mhagama amempongeza sana Rais Jakaya Kikwete kwa kuwaelezea watanzania kuuhusu Katiba ya nchi hii,siku ya kuuaga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka 2011.Na azima yake ya kuunda Tume ya kukusanaya maoni juu ya katiba.kwa maoni yake anauliza:-
- Je ni watanzania wangapi wameshaiona katiba ya Tanzania?
- Nakama wamekwisha iona ina rangi gani?
- Ni Tasisi ngapi zimekwisha pelekewa Katiba ya Nchi?
- Kama sivyo basi Jambo la katiba lisichukuliwe kama jambo rahisi kama wengi wanavyo lichukulia.
Kuhusu kuifanyia marekebisho Katiba yatafanyiwa marekebisho yepi ambayo wananchi wenyewe hawajawahi kuiona na kuyasoma yaliyomo na kusema sasa haya yafanyiwe marekebisho.
Kaongezea ili jambo hili lisiwe la watu wachache tu waliyobahatika kukutana na Katiba hiyo.Tume itakayo undwa kukusanya maoni iwe basi na nakala za kutosha za kuwaonyesha wananchi katiba hiyo ya zamani au elimu ya Uraia kuhusu katiba na yaliyomo yatolewe kwa wananchi ili wawe wanajua nini kinacho takiwa kufanyika ili kupata katiba itakayo wafaa watanzania.
Wanaotaka katiba mpya iundwe,je hiyo ya zamani wamekwisha iona na kuisoma hata kufikia mwafaka wa kuunda mpya?
Na kama ndivyo ni kweli kabisa katiba yote ya zamani haikuwa na jambo lolote bora kwa watanzania?
Pamoja na kuunda mpya lazima kuna baadhi ya vipengele vitakuwa na maana ni lazima vitabaki,watanzania lazima wawe waangalifu kuhusu jambo hili,kama midahalo kadhaa inayo endelea kuhusu Katiba,mambo mengi yataibuliwa,kila Tasisi itahusika,wananchi wakila hali watahitajiwa kutoa mawazo yao.
Je watatoa maoni kwa kitu wasichokijua? wala kukiona ?
Ili kutofautisha kitu kiomja na kingine ni lazima uvione kwanza vitu hivyo ndipo utoe kasoro.lakini katiba ya zamani watu hawajawahi kuiona wala kuisoma unamwambia toa maoni yako,unategemea kupata nini.
Maoni ya wasikilizaji wengine wapo tofauti na mawazo ya watu wanaodai kuwa suala la katiba lipelekwe Bungeni,watu wanasema Katiba si suala la kujadiliwa na wabunge peke yao,bali lipelekwe kwa wananchi ambao ndiyo wenye kuongozwa na katiba ya nchi,Hivyi suala la kukusanya maoni juu ya jambo hilo kutoka kwa wananchi ni la busara lisichukuliwe kama si jambo la muhimu.
No comments:
Post a Comment