Kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dkt Anselim Tarimo akizungumza na wanasemina ya wadau wa Ushirika mkoani Ruvuma katika ukumbi wa Songea Club leo
Dkt Tarimo aliyesimama akielezea umuhimu wa kutoa elimu ya ushirika na akiba ya kuweka na kukopa katika semina ya wadau wa Ushirika 80 kutoka wilaya za Tunduru,Namtumbo,Songea na Mbinga katika ukumbi wa Songea Club leo mwenye ngou nyekundu ni Kaimu Mratibu wa Mafunzo MUCCOBS Kituo cha Songea Bibi Benigna Filipo Haule.
Bibi Benigna Haule mwenye nguo nyekundu wakiteta jambo na Afisa Ushirika Mkoa BwanaWatson Nganiwa wa katikati na wa mwanzo kulia ni Elishan Emiliani Afisa masoko Mbinga kabla ya kuanza semina leo katika ukumbi wa Songea Club leo.
Mwenye kiti wa MUMSASICHEMA Tunduru Bwana Issa Kambutu akitoa shukrani kwa mgeni Rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Semina wa Muda bwana Hassani Daraja
Afisa masoko wa Mbinga Benki ya wananchi Bwana Elishan Emilian aliyeshika kipaza sauti akitoa mada juu ya benki yao inavyo wasaidia wananchi wa Wilaya ya Mbinga katika semina hiyo leo Songea Club katika Manispaa ya Songea leo
Meneja wa mikopo wa benki ya NMB tawi la Songea Bwana Derick Fidelis akitoa mada yake kwa wajumbe w semina ya wadau wa Ushiriki mkoani Ruvuma,kuhusu benki hiyo inavyo toa mikopo mbalimbali kwa wananchi.
Baadhi ya wjumbe wakimsikiliza MC wakati wa mapunziko madogo katika semina hiyo leo
Kaimu RAS Dkt Tarimo akielezea azima ya serikali kupeleka Ruzuku ya pombejeo ya wakulima moja kwa moja katika SACCOS zao wawe kama wakala,kupunguza wimbi la watu wasio waaminifu kuiba Vocha za pembejeo kwa kuziuza kwa bei ya hasara.
WANANCHI wa mkoa wa Ruvuma wametakiwa kujenga tabia ya kuweka akiba zao katika taasisi za kifedha zikiwemo mabenki ya CRDB,NMB,NBC,VICOBA na Benki ya Wananchi Wilaya ya Mbinga.
Akifungua semina ya wadau wa Ushirika mkoani Ruvuma Mgeni Rasm Kaimu RAS Dkt.Anselm Tarimo,alisema hayo leo katika ukumbi wa Songea Club kwa semina iliyoshirikisha wajumbe 80 kutoka Wilaya za Tunduru,Namtumbo,Songea na Mbinga.
Dkt Tarimo alisema kama watu wangeweka akiba zao wasingeweza kuuza Vocha zao za pembejeo za mbolea na mbegu kwa bei ya hasara,wakati serikali imeghrimia ili wakulima waweze kulima kitaalamu na lengo la kilmo kwanza lifanikiwe.
Aidha alisema elimu inayotolewa na Ushirika Mkoani Ruvuma ni muhimu sana kwa wananchi,kwani kuna miradi mingi itakayo waingizia wananchi fedha,hivyo ni muhimu wawe na elimu ya kuweka akiba katika mabenki.
Alitaja miradi hiyo kuwa ni ya barabara,madini ya Urenium na Makaa yam awe Namtumbo na Umeme wa Gridi ya Taifa unatarijiwa kujengwa hapo baadaye,wananchi wengi wataajiriwa na kupata fedha,hivyo wakiwa na elimu ya kuweka akiba zitawasaidia katika kununua pembejeo za kilimo.
Dkt Tarimo alisema Zuruku za pembejeo za kilimo zinazotolewa na serikali zitapelekwa kwenye SACOS.na SACOS za vijijini ndizo zitakazo kuwa wakala wa usambazaji wa pembejeo hizo za kilimo kupunguza wizi unaojitokeza kwa baadhi ya watu wasio waaminifu.
No comments:
Post a Comment