katika msimu huu wa mvua katika mikoa ya Ruvuma na Iringa wanaotumia pombe za kienyeji,maarufu kama komoni,kangara,ngerenge,mbege ingawa inatumika na wenyeji wa Kilimanjaro sasa ni maarufu pia katika mikoa hii.wataingia kwenye kinywaji maarufu kwa jina la ulanzi au ulai kwa wangoni.wenyeji wa Iringa ambao ni wahehe na wabena ulanzi ukilala kesho wanauita mkangafu,na ukiwa wajuzi watauita mdindifu maana ni pombe kali mmno.
mmea huu unakatwa machipukizi yake wakati yakianza kukua,basi wanaofanya kazi hiyo huitwa wagema,kama wanavyo sema kukimsifia mgema tembo hulitia maji' tembo ni pombe itokanayo na mnazi.lakini ulanzi unatokana na mianzi.lakini si kila mianzi inauwezo wa kutoa ulanzi au bamboo juice.
Uzuri wa pombe hii ni kwamba haihitaji kuwekwa kimea kutoka katika ulezi,matama ama shairi,hapana inakatwa mimea michanga jioni ama asubuhi na kufungwa na mianzi iliyokauka ambayo ule utonvu ama juice hujaa katika container hizo na kujaza katika chombo.lakini kabla ya mnywaji au mgema nyuki wao wanaanza kuonja kama ni kali.
No comments:
Post a Comment