Mganga Mkuu wa hospitali Mkoa Songea Dkt Daniel Malekela alisema siri ya kufanikisha ukarabati wa Hospital hiyo ya mkoa ni namna walivyo tumia mamilioni kadhaa yaliyotplewa na serikali kwa ajili ya kukarabati nyumba ya upasuaji,OPD sehemu ya juu,jengo la akinamama kwa ajili ya kujifungua pamoja na chumba cha upasuaji akinamama ambao hawana uwezo wa kujifungua kwa kawaida.
Alisema jengo lilokarabatiwa lina vitanda 80 vya kulaza wagonjwa waliofanyiwa upasuaji na wagonjwa wakawaida.Alisema kwa kufanya au kupata ushauri kutoka uongozi wa juu mkoani hasa Mhe.Salehe Pamba ambaye alikuwa RAS wa mkoa huo,na mkuu wa mkoa pamoja na uongozi wa taasisi ya hospitali hiyo ya mkoa ndiyo imefanya majengo yaonekane bora na kuvutia,hata mgonjwa anakuwa na matumaini ya kupona kabla hata ya kupata matibabu.
Hayo uliyosema katika kuhitimisha ujumbe wako, ingawa yanaonekana kama mchapo, yana ukweli, na watafiti wanathibitisha hilo. Uponaji wa mgonjwa sio suala la dawa tu, bali unachangiwa na masuala ya kisaikolojia, kama vile tabia za wahudumu, lugha wanayotumia, na mazingira ya hospitali.
ReplyDeleteshukrani kwa hilo kweli tupo pamoja ,unajua saikoloji ni jambo la muhimu sana kwa binadamu,mazingira na lugha za wauguzi wetu ni tiba tosha kwa mgonjwa,
ReplyDelete