Kaimu mkuu wa Kituo MUCCOBS Kituo cha Songea Bibi Benigna Filipo Haule akiwa katika ofisi ya muda baada ya kuezuliwa ofisi yaka Katika Manispaa ya Songea
Ofisi ya kituo cha Songea iliyo ezuliwa kufuatia upepo mkali na mvua ya tarehe 18 mwezi januari mwaka huu,iliyo karabatiwa ukuta uliyoanguka kama unavyo uona,walio simama wa kwanza kwenye tofali ni askari na anaefuatia ni Mkuu wa kituo hicho Bibi Benigna Haule akitoa maelekezo kwa mlinzi wake.
Mkuu wa Kituo Bibi Benigna Haule akiangalia jinsi mafundi wake walivyo jenga ukuta wa chuo hicho uliyo angushwa na Upepo uliyoandamana na mvua kali siku hiyo.
Hayo ni baadhi ya madirisha yaliyo tolewa katika chumba cha Mkuu wa kituo kilicho anguka siku hiyo wakiya hamishia katika darasa ambalo lina vifaa vya ofisi.
UPEPO mkali uliyeandamana na mvua mwezi januari tarehe 18 mwaka huu,umesababisha uharibifu wa mali na fifaa vya Kituo cha MCCoBS cha Ruvuma baada ya kuanguka ukuta wa kituo hicho.
Kaimu Mkuu wa kituo hicho Bibi Benigna Filipo Haule aliiambia Blog hii ofisini hivi karibuni kwake kuwa mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali uliangusha haadhi ya kuta za kituo hicho na kuacha mafaili na nyaraka mbalimbali za Serikali kulowana na mvua.
Alisema baada ya uharibifu huo vifaa vyote vilihamishiwa kwenye chumba cha darasa lakini hata chumba hicho si salama sana kwani kinavuja,ama mvua ya upepo kupitia madirishani kutokana na uchakavu uliyopo katika majengo ya kituo hicho.
Aidha Bibi haule alisema kuwa hatu za awali za kukinusuru kituo hicho jitihada za awali zimekwesha chukuliwa kwa kufanya ukarabati wa awali wa kuta zilizo athirika na upepo mkali wa mvua katika Manispaa ya Songea,uliyogharimu shilingi 1.066,000 ambazo zimishia ujenzi tu.
Alisema amekwisha taarifu wakuu wake na kufika uona uharibifu huo,na kuahidi kutoafedha za kufanyia ukarabati ofisi hiyo,kwa sababu inamlazimu kwenda ofsini hata siku za Juma pili kwa kuwa walinzi wengi wa mchana kutoka Kampuni ya Komesha Security Services LTD ni wanawake ambo ni rahisi kuvamiwa na kuporwa mali na vifaa vya ofisi.
Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara,kituo cha Ruvuma ni muhimu sana katika Mkoa wa Ruvuma kwani kinatoa mafunzo mbalimbali ya elimu ya ushirika na Ujasiliamali kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali,vyama vyaushirika vya akiba na mikopo,vyama vya mazao na uzalishaji kutoka wilaya za Tunduru,Namtumbo,Songea na Mbiga..
No comments:
Post a Comment