Monday, January 31, 2011

BREAKING NEWS,!!!!! PROFESA TIBAIJUKA AJA NA KALI ZIFUATAZO..

Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Ardhi Nyumba na makazi ,aja na zifuatazo:
  • Atakaye hamisha mawe (Bi cons)  ya mipaka ya kiwanja atakwenda jela miezi 6.
  • Askari wa Ardhi nyuma na makazi watafanya kazi hiyo ya kubaini uhalifua huo wa kuhamisha mawe Bi cons ) ya mipaka kwa tamaa ya kuongeza kiwanja.
  • kila mwananchi anahaki ya kupata Hati ya Ardhi kwa kufuata sheria bila njia za mkato (short cuts)
  • Maafisa ardhi wafanye kazi zao kwa kufuata sheria bila kukomoana.

BREAKING NEWS,PROFESA ANNA TIBAIJUKA AJA NA MPYWA KWA WAKAIDI WA KUNG'OA MAWE BIKONI

  1. a
  2. Mheshimiwa Profesa Anna Tibaijuka waziri wa Ardhi nyuma na makazi ,anasema kama askari wa usalama barabarani  Traffic wanaangalia uasalama barabarani kwanini basi kada ya askari wa Ardhi na makazi wasirejeshwe kazini. 
  3.  
    Askari wa ardhi na makazi warejeshwa kazini,ili kuangalia ukiukwaji wa sheria za ujenzi uliwekwa kisheria na serikali.

    Waziri wa Ardhi na makazi Mhe.Profesa Anna Tibaijuka alisema katika mahojiano na ITV kuwa kada hiyo ilisahaulika hapo awali lakini sasa watarudi kazini kwakuwa kuna watu wenye kiburi cha kung’oa mawe yanayowekwa kwa tamaa yakupanua kiwanja chake.

    Alisema kama mtu yupo tayari kuishi mjini basi afuate kanuni na sheria za ardhi za kuheshimu mipaka ya viwanja vyao.Hatupo hapa kwa kukomana bali tunafanya  kazi kwa kushirikiana na wananchi.

    Aidha alisema kutaundwa Programu ya kuwawezesha vijana nyumba au kiwanja,katoa mfano kupata nyumba Kinondoni ama kiwanja Bunju.

    Profesa Tibaijuka alisema anafanya kazi aliyopewa na Rais.na hafanyi kazi njia za mkato ( short cut ),short cut zimeshapitwa na wakati kitakacho takiwa ni kufuata sheria za ardhi na nyumba na makazi.pia lasema kazi katika sekta hiyo si ya kukomoana,bali ni kutoa elimu kwa wananchi ya kujua haki zao

TUJIFUNZE KUSINI WAPANGA MIKAKATI YAKE 2011

TUJIFUNZE yapanga mikakati kwa mwaka huu wa 2011,Baadhi ya watumishi wa TUJIFUNZE KUSINI wakiwa ofisini kwao wakitafakari changamoto kadhaa zilizojitokeza mwaka 2010, na kutafuta ufumbuzi wa kurekebisha changamoto hizo.Na kuanza upya shughuli ili kutekelza malingo waliyojipangia.

Dhana ya kuchimba dawa kwa wasafiri wa mabasi hakuhitaji Hotel au toilet

Hao ni wasafiri kutoka Songea kwenda Dar esa salaam,kama kilometa chache kufika Njombe Dereva wa Basi la Summry  alisimamisha busi na abiria wakaenda kujisaidia,na mara nyingi ni haja ndogo maarufu kwa jina la kuchima dawa. kuna kosa gani?
 
Sasa Dhana hiyo inazua mijadala kibao miongoni mwa watu,na wengine hawaja wahi kusafiri umbali mrefu kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 2 usiku ama siku mbili njani.Ikumbukwe basi linabeba abiria wakila sampuli,kuna wazee,watoto,wagonjwa ndiyo maana kuchimba dawa kutabakia kama kulivyo,kutokana na mazingira ya usafiri yalivyo.
 
Maoni ya wadau wengi wanadai wajenge maeneo maalumu ya kuchimba dawa hilo sipingi,daharula ikitokea kwa abira kushikwa tumbo la kuharisha na kituo cha kuchimba dawa kilicho andaliwa kiko mbali je huyo abiria atakuwa katika hali gani?

WATU SASA WATAPATA KILEVI KIKUBWA KWA KUNYWA ULANZI KWA FEDHA KIDOGO

katika msimu huu wa mvua katika mikoa ya Ruvuma na Iringa wanaotumia pombe za kienyeji,maarufu kama komoni,kangara,ngerenge,mbege ingawa inatumika na wenyeji wa Kilimanjaro sasa ni maarufu pia katika mikoa hii.wataingia kwenye kinywaji maarufu kwa jina la ulanzi au ulai kwa wangoni.wenyeji wa Iringa ambao ni wahehe na wabena ulanzi ukilala kesho wanauita mkangafu,na ukiwa wajuzi watauita mdindifu maana ni pombe kali mmno. 

mmea huu unakatwa machipukizi yake wakati yakianza kukua,basi wanaofanya kazi hiyo huitwa wagema,kama wanavyo sema kukimsifia mgema tembo hulitia maji' tembo ni pombe itokanayo na mnazi.lakini ulanzi unatokana na mianzi.lakini si kila mianzi inauwezo wa kutoa ulanzi au bamboo juice.

Uzuri wa pombe hii ni kwamba haihitaji kuwekwa kimea kutoka katika ulezi,matama ama shairi,hapana inakatwa mimea michanga jioni ama asubuhi na kufungwa na mianzi iliyokauka ambayo ule utonvu ama juice hujaa katika container  hizo na kujaza katika chombo.lakini kabla ya mnywaji au mgema nyuki wao wanaanza kuonja kama ni kali.

Sunday, January 30, 2011

huruma imatoweka miongoni wa watu katika jamii Duniani

 Huruma imetoweka miongoni mwa watu katika jamii,hayo yamesemwa leo katika mahubiri yake Rv Father Deogratias Nditi katika kanisa dogo kigango cha Matarawe Katika manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma.

Father Nditi alisema kwa jamii imekosa huruma,ndiyo maana hawaoneani huruma.Alisema mwaka huu matokeo ya kidato cha nne si mazuri katika Sekondari za kata,si kwa sababu shule hazina walimu wa kutosha na matatizo mengi,si hivyo tu bali kuna watoto wengine wamekosa vitabu,sare.chakula cha kutosha,huwenda hawana wazazi.au wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.Lakini watu wasio na huruma kwa watoto hawa wameshindwa kuwasaidia.hata mtu angetoa daftari tu lingemsadia,ili kupunguza wimbi la vijana wanaoshindwa mitihani yao na kuwa vibaka,na majambazi kwa kukosa kazi hapo baadaye. 
Kwaya ya Shirika la Kipapa likiimba wakati wa Ibada iliyoendeshwa na Padre Nditi katika kigango cha Matarawe leo,wakiwemo na viongozi wao walio wachagua  kwa kufuata Demokrasia.

SHIRIKA LA KIPAPA MATARAWE LAPATA VIONGOZI WAKE

 Shirika la Kipapa Kigangocha Matarawe kimepata viongozi wake,wakwanza kulia ni Charity  Gama  mwenye gauni  la Bluu Mwenye Kiti,anayefuatia mwenye nyeupe Charity Zeite ni Katibu mkuu.na mwenye gauni la dark blue Angela Mbithile mwenyekiti msaidizi na wa mwisho kulia mwenye gauni nyenkundu ni Agnes Hokororo ni mweke hazina.na Epifania Tolle mwenyekiti msaidizi hayupo kwenye picha.

Uongozi hauhitaji umri bali ni Imani ni kwa njinsi gani watu wanavyo mwamini,ndiyo maana watoto wa shirika la kipapa katika kigango cha Matarawe walivyo wachagua hao kuwa viongozi wao katika shirika lao.
Walezi wa watoto hao wa shirika hilo ni Bibi Beata Ponera mwenye gauni leusi na maua na Bibi  Lucy Mhagama mlezi msaidizi, Ndiyo wanaosimamia malezi ya watoto wa shirika la Kipapa kwa kuwa na rehema ya hali ya juu.

BINADAMU TUWE NA HURUMA KAMA ANAVYO TUHURUMIA MUNGU

Binadanu hatuhurumiani wenyewe kwa wenyewe,ni marangapi binadamu anaanguku kwa dhambi,anamkosea Mungu lakini Mungu anatoa msamaha,hayo ni baadhi ya mahubiri ya Padre ( Rv.Degratias Nditi ) Padre anayefundisha Seminari Kuu ya Peramiho katika Kigango cha Matarawe katika Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma leo.

Baba Padre Nditi  alirejea  MISALE YA WAUMINI Somo la leo '  Heri wenye Heri:' maana  hao watapata Rehema':ina maana wale ambao wanahuruma na wao watahurumiwa siku yaka.Ailsema huruma isipokuwepo na visasi vitatawala.' ni marangapi ukienda vijijini wananchi wanalalamika mazao yao yanakosa mbolea.wakati viongozi wasio na huruma wanagawa mboleakwa njia zisizo eleweka na kufurahia?' alisema.

Alisema nchi kama Tunisia wananchi wako katika machaufuko ya Kisiasa ni kwa sababu viongozi wao hawana huruma kwa wananchi wao,hali kama hiyo haiendi na mifano ya Mungu anayetuhurumia wakati sisi tuna mkosea,tunamchukiza kwa maovu tunayo mtendea kila mara.

Friday, January 28, 2011

IJUMAA YA LEO KARIBU KUSINI UKUTANE NA WAGENI KUTOKA WILAYA YA MBINGA MKOA WA RUVUMA

 Wageni wetu waliotutembelea katika ofisi yetu ya TUJIFUNZE KUSINI wakiwa walimu wa Sule ya Sekondari Makita Mbinga Mwalimu Atarasila B.Hyera anayeonyeshwa Gazeti la Tujifunze lililochapwa kwa rangi,na anaye fuatia ni mwalimu Euristar A.Ndunguru wakiwa katika ya Ofisi ya Mhariri Msaidizi wa TUJIFUNZE ,pia ni mwenye kiti wa Ruvuma Press Club Bwana Juma Nyumayo anaye onyesha Gazeti na mwenye suti ni Afisa Uzalishaji wa TUJIFUNZE Bwana Joram Mwaipopo.
 Hapa Bwana Juma Nyumayo  karibu na mashine akiwaonyesha wageni wake mtambo wa kuchapia gazeti la TUJIFUNZE na Jarida la Elimu (  Ed- SDP News Letter )
Wilaya ya Mbinga na mwambao wa Ziwa nyasa ambayo sasa ni wilaya mpya,kuna makabila ya Wamatengo,Wamanda,Wanyasa.wana ngoma maarufu sana kama Mhambo unayoiona wakicheza,hiyo ni ya wamatengo,kuna kioda kinachezwa na akina mama wa kimatengo Kimanda,pia kuna Mganda unaochezwa na Wanyasa na Wamatengo ili zimetofautiana katika uchezwaji wake.

NOTI MPYA ZA ZUA MJADALA MITAANI NA MASWALI MENGI NA MABISHANO

Hiyo ni baadhi ya Noti mpya zilizotolewa na  Benki kuu Tanzania ya Shilingi elfu 5 ( 5,000 ),na nyingine za shilingi elf moja ( 1,000 ) ,mbili ( 2,000 ) na Elfu kumi ( 10,000 ).Unajua ni nini kinasababisha mijadala na mabishaono kati ya watumiaji sokoni,dukani,na kwa wadau mbalimbali.

Watumiaji wengi wamezifia sana noti mpya kwakuwa ni ndogo ( Small size ),ambazo zinafaa kukaa katika pochi,wengine wanasema ni nyepesi mno zikitumika kwa muda mrefu zitachakaa sana,wengine wanasema rangi za noti hizo ni nzuri

Tuesday, January 25, 2011

HII NDIYO MAKUMBUSHO TA TAIFA YA MAJIMAJI SONGEA ( SONGEA NATIONAL MESEUM)

 Ndani ya jengo hilo kuna masalia na zana mbalimbali wangoni walikuwa wakitumia ni pamoja makabila yote ya mkoa wa Ruvuma vya utamaduni wao,
 Hiyo ni nyumba ya kimila ya wangoni ambayo wangoni walikuwa wakijenga katika  Kingdom  zao waliosimama ni wa zee wa kimila wa kingoni mwenye kaunda suti ni mzee John Joseph Gama Makamu mwenye kiti wa Makumbusho ya Majimaji. wapili mwenye kamtule ni mzee  Crispin creophas Mahuna.
 Hilo hapo ni kaburi la cheif wa kingoni Songea  Luwafu Mbano ambaye alizikwa pekeyake katika kaburi hilo.
  hilo ni kaburi lililo zikwa machifu,nduna 66 katka kaburi moja ( kaburi la halaiki) Mass grave.
 Hiyo ni sanamu inayo wakilisha askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania waliokufa katika vita vya Idd Amin wa Uganda
Hapo ni ofisini kwa mkurugenzi wa makumbusho hayo Bwana Philip maligisu aliye vaa nguo nyeusi nakaimu mwenyekiti Mzee Joseph Gama mwenye kofia aliyeshika kitabu akimkabidhi Mwenye kiti wa Press Club Ruvuma Bwana Juma Nyumayo hayupo taika picha.



Makumbusho ya Taifa ya Majimaji yana madhumuni ya kutunza,kuhifadhi ulithi na utamaduni wa mtanzania.

Madhumuni mengine ni Taasisi ya makumbusho ya taifa kama mhifadhi namba moja wa urithi wa mtanazia.

Mkurugenzi wa Makumbusho ya majimaji Bwana Philip Maligisu anasema kazi zilizopo katika makumbusho hayo ni pamoja na kukusanya rasilimali za utamaduni wa mtanzaia.

Pia pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu urithi wa utamaduni wa asili,kufanya utafiti na kuhifadhi kumbukumbu muhimu ili ziwe salama kwa niaba ya Umma.

Kushirikisha watanzania kupitia Program za utamaduni ili kuonyesha jamii utamaduni wa mtanzania,ili kufungua mtandao mpana wa ndani na nje ya nchi ( Network system ).

Pia wananchi waweze kuelewa na kuanzisha makumbusho ya Taifa katika wilaya ambapo tarehe 22 hadi 23 wadau wa makumbusho watakwenda wilaya ya Mbinga kuanzisha makumbusho ya Taifa katika wilaya hiyo mkoani Ruruma kwakuwa wao wamesha fikia katka sifa ya kuanza makumbusho yao.

Kwa kuwa wilaya hiyo itakuwa karibu na wilaya mpya ya Nyasa wataweza kupanua utalii kupitia ziwa nyasa,makaa ya mawe na uoto wa asili ambao utawavutia watalii..

Bwana Philip alisema makumbusho haya yalianza kabla ya ukoloni kwa sheria namba 40 ya mwaka 1936,na baadaye kutungwa sheria  Tanganyka namba 23 ya mwaka 1963  baada ya Uhuru.

Na baadaye sheria namba 37 ya mwaka 1965  ambayo ilikuwa na waziri mwenye Dhamana na makumbusho ya taifa na hatimaye seria namba 7 ya mwaka 1980 yakuwa na makumbusho ta Taifa ambayo yapo Dar es salam.

Makumbusho ya taifa ya  majimaji yatafungua wigo wa watalii kutembele Songe kuona wanya katika hifadhi ya Seluu,Ruhira ambako kuna hifadhi ya wanyama kama vile viboko na ndege wenye rangi za kuvutia.

IJUE MAKUMBUSHO YA TAIFA YA MAJIMAJI KATIKA MANISPAA YA SONGEA

 Wazee wa kingoni wakicheza ngoma yao ya ligihu ambayo ilachezwa na wazulu wa Afrika kusini.ngoma hii ni maarufu inachezwa wakati wa sherehe na matukio ya kuonyesha jadi ya wangoni na walikotokea.
 Ngoma hiyo huchezwa na wazee wakiume na kike wakiwa wameshika kishoka kwa kingoni ni kinjenje na ngao iliyotengenezwa kwa ngozi ikiwa ni kama kifaa cha kuzuia mkuki au kinjenje kisimkate.kwa kukinga kwa adui wake.
Hawa walitoka Afrika ya kusini wakiukimbia utawala wa Chaka Zulu na kuelekea Zimbabwe na matawi mengine yalifika Tanzania

SOKO LA KITI MOTO / LIGULUWI/BEKENI/AU PORKMANISPAA YA SONGEA LAVYAMIWA NA WACHINA

Soko la nyama ya nguruwe kwa jina maarufu kiti moto au Liguluwi ama pork limevamiwa na wachina wanaojenga barabara ya Millennial  Challenge  ya kuanzia Peramiho hadi mbinga,kwani wachina hao hufika Songea na kununua nguruwe wazimawazima.

kutokana na uvamizi huo kilo moja ya kitimoto imepaa kutoka shilingi 3,500 hadi shilingi 6,000.kutokana na kupaa huko kwa bei nyama hiyo wateja wameanza kupongua wanako andaa kwa utaalamu zaidi,Makukula,Makondeko,Songea girls,Matogoro na Bombambili.

wezi wa vucha za pembejeo Songea kesho mahakamani,kilio cha wakulima kimesikika

 Watu wanne watafikishwa mahakamani kesho kufuatia kuibiwa vocha za pembejeo 4,599 zenye thamani ya shilingi 21,114,000.Pembejeo amazo zilitakiwa kupelekwa katika kata 21 lakini kati ya kata hizo kata 9 zimekosa vocha hizo.

Watakao pelekwa mahakamani kesho ni pamoja na Afisa  kilimo na mifugo wa Manispaa ya Songea Dkt Frenk Nkoma ,Michaela matembo Mratibu wa Pembejeo wa Manispaa ya Songea,Dani Kagema Mhasibu msaidizi wa Halmashauri hiyo na wakala wa pembejeo Bwana Prosper Mahai.

Inadaiwa kwa katika  Kata ya Subira,zilitakiwa kupelekwa vocha 174 lakini hazikupelekwa,Kata ya Lilambo zilitakiwa kupelekwa vocha 120 lakini zimepelekwa vocha 30 tu,Kata ya Lugagala  zilitakiwa kupelekwa vocha 100 lakini zimepelkwa 50 tu..
Nyingine ni kata ya kilagano zilitakiwa kupelekwa vocha 130 lakini zimepelekwa vocha 30 tu,na Mlete palitakiwa kupelekwa vocha 122 lakini vocha zilizofikishwa katani hapo ni 50,kufuatia kubainika kwa mgao huo wa vocha hizo polisi wanafuatilia mgawanyo huo.

'Wananchi wa Songea na Mkoa mzima ambao ni wakulima wanaopata shida ya  pembejeo kilio chao kimesikilizwa na Mungu; alisema mkulima mmoja ambaye hakutaka ajulikane katika Blog hii.

Upepo na mvua ya sababisha vifaa vya Chuo cha Ushirika Songea kuwekwa darasani

 Bibi Benigna Filipo Haule akionyesha baadhi ya typewriter ambayo hutumika kufanyia kazi katika ofisi hiyo,baada ya computer za kituo hicho kuibiwa kufuatia wizi mdogo mdogo unaofanyika kutoka na ubovu wa ofisi hiyo.
 Hivyo ni vifaa na nyaraka za ofisi ya mkuu wa kituo hicho MUCCOBS Ruvuma kufuatia maafa ya mvua tarehe 18 mwezi huu mwaka 2011.uliyo sababisha nyumba nyingi za wakazi Manispaa ya Songea kuezuliwa na nyingine kuanguka.
kaimu mkuu wa chuo hicho Bibi Benigna Filipo haule akionyesha jinsi upepo ulivyo sababisha dari ya darasa lililo hifadhiwa vifaa vya ofisi vikiwemo vyaraka kadhaa za chuo hicho MUCCOBS Ruvuma Katika Manispaa ya Songea.

OFISI ya MUCCoBS Kituo cha Songea yaangushwa na upepo

 Kaimu mkuu wa Kituo MUCCOBS Kituo cha Songea Bibi Benigna Filipo Haule akiwa katika ofisi ya muda baada ya kuezuliwa ofisi yaka Katika Manispaa ya Songea

 Ofisi ya kituo cha Songea  iliyo ezuliwa kufuatia upepo mkali na mvua ya tarehe 18 mwezi januari mwaka huu,iliyo karabatiwa ukuta uliyoanguka kama unavyo uona,walio simama wa kwanza kwenye tofali ni askari na anaefuatia ni Mkuu wa kituo hicho Bibi Benigna Haule akitoa maelekezo kwa mlinzi wake.
 Mkuu wa Kituo Bibi Benigna Haule akiangalia jinsi mafundi wake walivyo jenga ukuta wa chuo hicho uliyo angushwa na Upepo uliyoandamana na mvua kali siku hiyo.
Hayo ni baadhi ya madirisha yaliyo tolewa katika chumba cha Mkuu wa kituo kilicho anguka siku hiyo wakiya hamishia katika darasa ambalo lina vifaa vya ofisi.



UPEPO mkali uliyeandamana na mvua mwezi januari tarehe 18 mwaka huu,umesababisha uharibifu wa  mali na fifaa vya Kituo cha MCCoBS cha Ruvuma baada ya kuanguka ukuta wa kituo hicho.

Kaimu Mkuu wa kituo hicho Bibi Benigna Filipo Haule aliiambia Blog hii ofisini  hivi karibuni kwake kuwa mvua hiyo iliyoambatana na upepo mkali uliangusha haadhi ya kuta za kituo hicho na kuacha mafaili na nyaraka mbalimbali za Serikali kulowana na mvua.

Alisema baada ya uharibifu huo vifaa vyote vilihamishiwa kwenye chumba cha darasa lakini hata chumba hicho si salama sana kwani kinavuja,ama mvua ya upepo kupitia madirishani kutokana na uchakavu uliyopo katika majengo ya kituo hicho.

Aidha Bibi haule alisema kuwa hatu za awali za kukinusuru kituo hicho jitihada za awali zimekwesha chukuliwa kwa kufanya ukarabati wa awali wa kuta zilizo athirika na upepo mkali wa mvua katika Manispaa ya Songea,uliyogharimu shilingi 1.066,000 ambazo zimishia ujenzi tu.

Alisema amekwisha taarifu wakuu wake na kufika uona uharibifu huo,na kuahidi kutoafedha za kufanyia ukarabati ofisi hiyo,kwa sababu inamlazimu kwenda ofsini hata siku za Juma pili kwa kuwa walinzi wengi wa mchana kutoka Kampuni ya Komesha Security Services LTD ni wanawake ambo ni rahisi kuvamiwa na kuporwa mali na vifaa vya ofisi.

Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Biashara,kituo cha Ruvuma ni muhimu sana katika Mkoa wa Ruvuma kwani kinatoa mafunzo mbalimbali ya elimu ya ushirika na Ujasiliamali kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali,vyama vyaushirika vya  akiba na mikopo,vyama vya mazao na uzalishaji kutoka wilaya za Tunduru,Namtumbo,Songea na Mbiga..



Sunday, January 23, 2011

BREAKING NEWS, KIZAZA SPOTS ITV ,LEO

Ni nani mwenye viwanja vya micheo nchini TFF,SERIKALI AU CCM.na kwanini kiwango cha soka letu kinashuka kila kukicha?

Je viwanja vyetu viko  kwenye hali nzuri? viko katika viwango vinafikia  kuitwa kiwanja cha mpira wa mguu?

JUMAPILI YA LEO NIMEKULETEA UONE MAENDELEO YA NA CHANGAMOTO ZA MJI WA SONGEA.

 Hayo ni mazingira ya standi yetu ya mabasi yaendayo nje ya mkoa wa Ruvuma  na jinsi inavyoonekana.mabasi yanaenda Dar es salaam,Mbeya,Iringa,Mbinga,Tunduru,Pamoja Taxi yanapatikana katika standi hiyo
 Huu ni moja ya mitaa ya mji wa Songea
vijana hawa wako katika harakati za kujipatia kipato kwa kuuza mananasi,wanasema mananasi hayo yanatoka Chalinze Kibaha,mengine Morogoro kwa hiyo inawalazimu kuuza kwa bei ya juu ili kupata faida,kuanzia shilingi 1,000/= hadi 2,000/=

SERIKALI KATIKA KUTEKELEZA KAULI MBIU YA KILIMO KWANZA INAZIDI KULETA PEMBEJEO ZA KILIMO SONGEA

Lori hilo lina shehena ya mbolea kwa ajili ya kukuzia mahindi mkoani Ruvuma katika wilaya zake za Tunduru,Namtumbo,Songea,Mbinga na wilaya mpya ya Nyasa.

Lori kama hilo  yanaingia mkoani hapa  ili kukidhi mahitaji ya wakulima,ila tatizo mbolea ya Ruzuku unayotolewa kwa wakulima haitoshelezi,kwani mfuko mmoja wa kilo 25 hautoshi kuweka katikaheka moja.wakulima wanaiomba serikali kutoa mifuko 3 ya mbolea  ya kupandia kwa mkulima mmoja.

Saturday, January 22, 2011

IJUE TUJIFUNZE KUSINI

TUJIFUNZE KUSINI ni kati ya Magazeti ya elimu ya watu wazima ya Kanda za elimu Saba nchini

Gazeti hili hutolewa na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuchapwa na kituo cha uchapaji S.L.P.712 SONGEA.

zikiwemo kanda za Kusini,Nyanda za Juu Kusini,Mashariki,Kaskazini,Kati ,Magharibi na Kanda ya Ziwa.

WANANCHI WA TUNDURU WAHAIDIWA HUDUMA YA BENKI YA CRDB

 Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Songea Bwana Gerald  Michael akitoa mada kwenye semina ya siku moja ya wadau wa Ushirika katika ukumbi wa Songea club
 Wajumbe wakisikiliza mada kuhusu huduma za benki ya CRDB
 Wajumbe wa semina ya siku moja ya wadau wa Ushirika wakijitambulisha kwa kikundi kwa mgeni rami
 Wajumbe wakijitambulisha kwa vikundi kwa mgeni rasmi katika ukumbi wa Songea club katika Manispaa ya Songea Leo
Mgeni Rasmi kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dkt Anselim Tarimo akisistiza umuhimu wa wananchi kupata elimu ya ushirika wa kuweka na kukopa,ili waweze kununu pembejeo za kilimo.ambapo Tunduru wanazao la korosho.Namtumbo tumbaku na Mbinga kahawa.

Naye 
Afisa wa Benki ya CRDB Tawi la Songea aliyemwakilisha Meneja wa Benki hiyo kwenye semina ya siku moja ya wadau wa ushirika mkoani Ruvuma leo Bwana Gerald Michael aliwaambia wanasemina wapatao 80 waliohudhuria semina hiyo kuwa Tayayari Jengo la huduma za kibenki linafanyiwa ukarabati wilayani humo. Alipojibu swali la mjumbe mmoja wa Tunduru.

Bwana Michael alisema huduma zao ni za uhakika na za usalama wa hali ya juu,isitoshe wanatoa mikopo kwenye SACCOS na wafanya kazi ambao waajiri wao wameingia mkataba nao.

Alisema hayo wakati akitoa mada yake kuhusu huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB kwa washiriki kutoka vyama vya ushirika,SACCOS,VIKOBA,na taasisi nyingine za kifedha na vyama vya ushirika vya kuweka na kukopa.

WATU WAWE NA TABIA YA KUWEKA AKIBA KATIKA MABENKI

 Kaimu RAS wa mkoa wa Ruvuma Dkt Anselim Tarimo akizungumza na wanasemina ya wadau wa Ushirika mkoani Ruvuma katika ukumbi wa Songea Club leo
 Dkt Tarimo aliyesimama  akielezea umuhimu wa kutoa elimu ya ushirika na akiba ya kuweka na kukopa katika semina ya wadau wa Ushirika 80 kutoka wilaya za Tunduru,Namtumbo,Songea na Mbinga katika ukumbi wa Songea Club leo mwenye ngou nyekundu ni Kaimu Mratibu wa Mafunzo MUCCOBS  Kituo cha Songea Bibi Benigna Filipo Haule.
 Bibi Benigna Haule  mwenye nguo nyekundu wakiteta jambo na Afisa Ushirika Mkoa BwanaWatson Nganiwa wa katikati na wa mwanzo kulia ni Elishan  Emiliani Afisa masoko Mbinga kabla ya kuanza semina leo katika ukumbi wa Songea Club leo.
 Mwenye kiti wa MUMSASICHEMA Tunduru Bwana Issa Kambutu akitoa shukrani kwa mgeni Rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Semina wa Muda bwana Hassani Daraja
 Afisa masoko wa Mbinga Benki ya wananchi Bwana Elishan Emilian aliyeshika kipaza sauti akitoa mada juu ya benki yao inavyo wasaidia wananchi wa Wilaya ya Mbinga katika semina hiyo leo Songea Club katika Manispaa ya Songea leo
 Meneja wa mikopo wa benki ya NMB tawi la Songea Bwana Derick Fidelis akitoa mada yake kwa wajumbe w semina ya wadau wa Ushiriki mkoani Ruvuma,kuhusu benki hiyo inavyo toa mikopo mbalimbali kwa wananchi.

 Baadhi ya wjumbe wakimsikiliza MC wakati wa mapunziko madogo katika semina hiyo leo
Kaimu RAS Dkt Tarimo akielezea azima ya serikali kupeleka Ruzuku ya pombejeo ya wakulima moja kwa moja katika SACCOS zao wawe kama wakala,kupunguza wimbi la watu wasio waaminifu kuiba Vocha za pembejeo kwa kuziuza kwa bei ya hasara.


WANANCHI wa mkoa wa Ruvuma wametakiwa kujenga tabia ya kuweka akiba zao katika taasisi za kifedha zikiwemo mabenki ya CRDB,NMB,NBC,VICOBA na Benki ya Wananchi Wilaya ya Mbinga.

Akifungua semina ya wadau wa Ushirika mkoani Ruvuma Mgeni Rasm Kaimu RAS Dkt.Anselm Tarimo,alisema hayo leo katika ukumbi wa Songea Club kwa semina iliyoshirikisha wajumbe 80 kutoka Wilaya za Tunduru,Namtumbo,Songea na Mbinga.

Dkt Tarimo alisema kama watu wangeweka akiba zao wasingeweza kuuza Vocha zao za pembejeo za mbolea na mbegu kwa bei ya hasara,wakati serikali imeghrimia ili wakulima waweze kulima kitaalamu na lengo la kilmo kwanza lifanikiwe.

Aidha alisema elimu inayotolewa na Ushirika Mkoani Ruvuma ni muhimu sana kwa wananchi,kwani kuna miradi mingi itakayo waingizia wananchi fedha,hivyo ni muhimu wawe na elimu ya kuweka akiba katika mabenki.

Alitaja miradi hiyo kuwa ni ya barabara,madini ya Urenium na Makaa yam awe Namtumbo na Umeme wa Gridi ya Taifa unatarijiwa kujengwa hapo  baadaye,wananchi wengi wataajiriwa na kupata fedha,hivyo wakiwa na elimu ya kuweka akiba zitawasaidia katika kununua pembejeo za kilimo.

Dkt Tarimo alisema Zuruku za pembejeo za kilimo zinazotolewa na serikali zitapelekwa kwenye SACOS.na SACOS za vijijini ndizo zitakazo kuwa wakala wa usambazaji wa pembejeo hizo za kilimo kupunguza wizi unaojitokeza kwa baadhi ya watu wasio waaminifu.