Waziri wa Kazi na Ajira Mhe.Gaudensia kabaka akihutubia maelfu ya wafanyakazi katika uwanja wa majimaji Katika Manispaa ya Songea leo katika kilele cha maadhimisho ya 8 ya usalama na afya kazini
Waziri katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanya kazi
Waziri na vikombe kabl haja kabidhi kwa washindi hapo chini.
Waziri akimkabidhi kikombe cha ushindi wa jumla Bw.Isack SenyaWaziri na vikombe kabl haja kabidhi kwa washindi hapo chini.
Ajali kazini husababisha hasara na kupunguza uzalishaji –
Kabaka
KILA mwaka serikali imekuwa ikipoteza wafanyakazi wake kwa kupoteza
maisha au sehemu za viungo vyao vya mwili katika sehemu zao za kazi pengine
bila ya kuwa na taarifa kutoka kwa wa waajiri,vyama vya wafanyakazi kwa
kutokuwa na takwimu za watu walioathirika mahali pa kazi.
Waziri wa kazi na Ajira Mhe. Gaudensia Kabaka alisema hayo siku ya
maadhimisho ya 8 ya usalama na afya kazini yaliyo fanyika kitaifa Mjini Songea
katika uwanja wa majimaji leo.
Mhe.Kabaka alisema Serikali,waajiri
na wafanya kazi pamoja na vyama vya wafanyakazi lazima kuzingatia kanuni zilizo wekwa na
Shirika la Kazi Duniani ( ILO ) la kuwa na sheria zitakazofuatwa. Za usalama na
afya kazini.
Alisema ukiona watu hawaendi
kazini kila mara ujuwe sehemu hiyo si salama,hivyo kuwe na kanuni na sheria
zitakazo fuatwa na kila mfanya kazi na kuwa na vifaa vya kujikinga na ajali
hasa sehemu za ujenzi,migodi na kwenye viwanda.ili kupunguza ajali.
Baada ya kufunga maadhimisho hayo
Mhe.Kabaka aligawa zawadi kwenye makampuni tisa ambayo yameonyesha umahili wao
katika usalama na afya kazini ,zawadi hizo likuwemo vikombe pamoja na vyeti.
No comments:
Post a Comment