Thursday, April 28, 2011

SERIKALI ITOE VIFAA VYA KINGA KAZINI KUEPUSHA AJALI MGAYA

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bwana Nicholaus Mgaya  asema serikali,waajiri na wafanyakazi wazingatie sheria zilizoainishwa na Shirika la kazi Duniani 
(ILO ) za usalama na afya kazini ili kupunguza ajali na magonjwa yanayo tokea sehemu za kazi.

Bw.Mgaya alisema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya usalama na afya kazini kitaifa zilizofanyika Mkoani Ruvuma katika manispaa ya Songea uwanja wa maji maji leo.

Aidha alisema ni muhimu serikali  na waajiri kuwa na vifaa vya kinga za ajali kazini na kutoa elimu  na mafunzo sehemu za kazi.

No comments:

Post a Comment