Mwakilishi wa Shirika la Kazi Duniani Bwana Magnus Minja akisoma hotuba ya Bwana Alexio Musindo,Mkurugenzi wa ILO Ofisi ya Tanznaia,Kenya ,Uganda na Rwanda wakati wa maadhimisho ya usalama na afya kazini tarehe 28 mwezi huu Songea Mkoa wa Ruvuma
SHIRIKA
la kazi Duniani ( ILO ) laipongeza serikali ya Tanzania kwa kuwa tayari na sheria
ya usalama na afya kazini mwaka 2003 ambapo mikakati inaendelea ya uhakiki wa
utekelezaji wake.
Mwakilishi
wa Shirika la kazi Duniani Bwana magnus Minja alisema hayo kwenye kilele cha
maadhimisho ya usalama na afya kazini kilichofanyika mkoani Ruvuma
tarehe 28 mwezi huu.
Bw.Magnus
alisema kuwa Tanzania
imekwisharidhia baadhi ya mikataba inayohusiana na usalama na afya kazini ambayo
ni mikataba Na..148 wa mwaka 1977 unaohusu mazingira ya kazi,Na.152 wa mwaka
1979 unaohusu usalama na afya kazini,kazi za bandarini na ule wa Na.170 wa mwaka 1990 unaohusu matumizi ya
kemikali.
Alisema
ni matarajio ya Shirika hilo
kuwa juhudi za serikali na wadau wengine wataendelea kuchukua jitihada zaidi
ili kuridhia mikataba mingine iliyobakia ukiwemo mkataba Na.187 wa mwaka
2006.Pamoja kuwepo kwa masharti ya usalama kazini hasa kwenye makampuni
makubwa,pia kuyasaidia makampuni madogo katika utekelezaji wake kwa vitendo.
No comments:
Post a Comment