Sunday, April 24, 2011

UFUFUKO WA YESU KRISTU ULETE AMANI,UMOJANA NA MSHIKAMANO MIONGONI MWA WATANZANIA

 Heri ya pasaka kwa watu wote Duniani kwaa  wanao mwamini na wasio mwamini,Padre Adam Mbando wa Parokia ya Makole Manispaa ya Dodoma akiwa mbele ya Altare akisubiri vipaji.' Ufufuko wa Yesu Kristo ni ishara ya uko mbozi wa binadamu wenye dhambi,hivyo watu wazidi kusali sana ili kuiombea nchi yetu maana kunajitokeza matendo yanayoonyesha uvunjifu wa amani' Alisema Padre Mbando.
 Aleluye Bwana amefufuka,aleluya imeenea duniani kote kwa watu wenye mapenzi mema.Padre Adam mbando wa Parokia ya Makole Manispaa ya Dodoma,Amesema watu wanatakiwa wafufuke na Bwana wetu Yesu Kristo.Alisema Baadhi ya Wa- tanzania wanataka kuharibu kisiwa chetu cha Amani cha Tanzania.
Amani ikikosekana ubinadamu unapungua,Yesu Kristo aliteswa kisha akafa,siku ya tatu alifufuka,kuonyesha utukufu wake,na hakuna ufufuko bila ya kifo,na hakuna kalvari bila ya kuteswa.Na umaskini wa watanzania sio ni laana tuliyopewa na Mungu,hapana bali ni ukosefu wa uwezo wa kutumia rasilimali zilizopo, kwa wale waliopewa dhamana ya kuongoza nchi.
 
 Kwaya ya Mtakatifu Kaloli lwanga iliyo kolezea Ibada ya Pasaka ya asubuhi katika kanisa la parokia ya Makole katika Manispaa ya Dodoma na Mkesha wa Pasaka.
Honhera zao wanakwaya hao Mungu awabariki wazidi kukoleza katika Ibada mbalimbali katika Parokia ya Makole.

No comments:

Post a Comment