Wednesday, April 13, 2011

HONGERA SERIKALI YA MKOA WA MOROGORO KUJENGA SEKONDARI YA UKUMBOSHO WA SOKOINE

Naipongeza Serikali ya mkoa wa Morogoro kushirikiana na Wilaya ya Mvomero kuandaa Bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari itakayo pewa jina la Sokoine Memorial High Secondary School eneo alilofia aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine Wami Ruhinda.

Sekondari ya kidato cha tano na sita itakyo sajili wanafunzi kutoka mikoa yote nchini.Ni vyema basi na Serikali za mikoa mingine Tanzania kuiga mfano huo mzuri ulio fanywa na Serikali ya Mkoa wa Morogoro kufanya kitu cha ukumbusho wa maisha.

Cha ajabu na cha kushangaza kuna baadhi ya viongozi mashuhuri katika mikoa fulani walionyesha juhudi zao katika uongozi na Mungu amewaita mbele za haki hawakufanyiwa kama ilivyo fanya Serikali ya Mkoa wa Morogoro.

Mfano mzuri na rahisi sana, Aliyekuwa Mbunge wa Songea Mjini Hayati Raurence Mtazama Gama ,Alifanya mambo mengi ya maendeleo katika mkoa wa Ruvuma,hadi leo wanasua sua kumpatia kitu chochote jina kama kumbu kumbu Mzee Gama.


Kuna shule ya sekondari inayojengwa Wilaya ya Namtumbo ya kidato cha tano na sita inayojengwa kwa ushirikiano wa wilaya zote za mkoa wa Ruvuma,Afisa Elimu wa mkoa huo alipendekeza sekondari hiyo iitwe Jina la Gama kumuenzi kutokana na juhudi alizozionyesha wakati alivyo kuwa mkuu wa mkoa huo,kilicho tokea huwezi kuamini baadhi ya wabunge alikataa kata kata kupewa sekondari hiyi jina la Gama. Makubwa wenyewe kwa wenyewe wanakataana.


No comments:

Post a Comment