Thursday, April 28, 2011

SHIRIKA LA KAZI DUNIANI ILO LAUNGANA NA SERIKALI YA TANZANIA LEO KATIKA MAADHIMISHO YA USALAMA NA AFYA KAZINI SONGEA RUVUMA

Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani ( ILO ) Bwana Magunus Minja akitoa maelezo ya malengo ya Shirika hilo kwa usalama na afya kazini ili kuepusha ajali na vifo kwa wafanyakazi Duniani.


MAADHIMISHO ya siku ya Usalama na Afya kazini Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Majimaji katika Manispaa ya Songea,Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudensia Kabaka ,baada ya kufunga maadhisho hayo alitoa zawadi katika taasisi 9 zilizo dhibiti viashiria vya usalama katika kazini.

  Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani Bwana Magunusi Mijna alisema,  Serikali ya Tanzania leo imeungana na Shirika la Kazi Duniani ( ILO) waajiri,na awafanyakazi  pamoja na vyama vyao vinavyo simamia utamaduni wa usalama na afya sehemu za kazi,yenye kauli mbiu “ Usimamizi wa usalama na afya: Zana ya uboreshaji endelevu”

Bwa.Minja alisema kuwa mwaka huu tunaadhimisha miaka 92 ya ILO kushughulikia haki katika jamii,kulinda  maisha na afya ya wafanyakazi wote ikiwa ni sehemu ya lengo pana la ILO la kazi yenye staha sehemu za kazi.

Alisema kwa kunukuu kuwa “Kulingana na azimio la Seoul la mwaka 2008 kuwa utamaduni wa taifa wa kulinda usalama na afya ni ule ambapo haki ya usalama na afya kazini inaheshimiwa katika ngazi zote,ambapo serikali ,waajiri, na wafanyakazi wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha mazingira hayo.

Bw.Minja alisisitiza kuwa kazi isiyo salama ni janga  la binadamu,ambayo husababisha  ajali,magonjwa na kupunguza uwezo wa kufanya kazi na kufupisha maisha ya mfanyakazi.Ambapo kila mwaka mamilioni ya majanga hutokea bilia kuripotiwa.

  Aidha alisema ili mfanya kazi awe salama mahali pa kazi ni budi kufuata mifumo ya  ( OSHMS ),kwa kuzingatia na  kuandaa Sera ya taifa ya usalama kazini  na kuweka miundombinu ya utekelezaji wa Sera na Programu zilizoandaliwa ,Programu ya taifa ya usalama na afya kazini kwa kuwa na  malengo ya kitaifa kwa muda uliyo pangwa.

Alisema ingawa ajali haina kinga lakini tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na mfanyakazi mwenyewe panapo tokea viashiria vya hatari sehemu ya kazi,kutoa elimu na mafunzo ana kuzingatia sheria zilizowekwa na  Serikali, vyama vya wafanyakazi,waajiri wafanyakazi na mashirika ya kijamii,ili kazi isiwe ya kufupisha maisha bali iwaongezee maisha wafayakazi.

No comments:

Post a Comment