Wednesday, April 20, 2011

HABARI KWA UFUPI KITENGO CHA HABARI,ELIMU NA MAWASILIANO KUANDAA TOLEO MAALUMU ARINE MOROGORO

 Ni siku ya kwanza kabisa baada ya wajumbe wote kuwasili katika hotel ya Arine Inn eneo la Kola hill Morogoro.
 Kitengo cha Habari ,Elimu na Mawasiliano na Wahariri wa Jarida la  Elimu Tanzania (Ed- SDP ) wa kanda saba za Elimu Tanzania huwa wakikutana kuandaa Jarida hilo  Mkoani Morogoro ili kuandika mambo muhimu kuhusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.Wakwanza ni Mhariri wa Moshi kilimanjaro na Oliva kato wa Kitango cha habari wakiandika habari.
 Mhariri Mstaafu wa tabora Bwana Lucas Ndanga wa kwanza na Kaimu Mhariri wa Morogoro Bwana Jems Tem wakiwa katika kuandika habari.
 Baandaa ya kuchambua na kuandika habari hizo zimepelekwa kwenye Computer kwa Lyaout ambapo Dada Oliva kato akiwa kwenye Computer,Mratibu Msaidizi Bwana Ntambi Buyanzu,akisoma kwa masahihisho ambapoElizabeth Pangras mwenye bauni lenye maua akihakiki.
 Wahudumu wa Hotel hii wakiwa tayari kwa  mahanjumati kwa wanahabari hao baada ya kazi maalumu
Hapa na mie nikiwa na wanahabari wenzangu tukitoka Arine Inn kuelekea tulikofikia hapa Mjini morogoro

No comments:

Post a Comment