Monday, April 11, 2011

BREAKING NEWS ! ! ! MSWADA WA MAREKEBISHO YA KATIBA UNALETE PICHA GANI KWA WATANZANIA?

Ni jambo la kutia wasiwasi sana kwa matukio yaliotokea Dodoma na Dar es salaam ya vurugu hata vyombo vya dola kutuliza ghasia.
 Lakini kwanini mswada huo ulichanwa hadharani Zanzibar na wajumbe wote kuukataa na kushangilia unapochanwa.
Hivyo ni kweli Muungano huu wanaukubali wananchi wa visiwani?,je hata serikali ya umoja wa kitaifa  upo kweli Visiwani?.

  Marekebisho ya mswada wa katiba mbona unaleta picha gani nchini?.

Hivyo wasomi hawawezi kufanya kazi hiyo badala ya wananchi,haiwezekani kila mmoja atake kitu chake kiwe kwenye katiba  na kiandikwe si itakuwa fujo?


Basi kama ni kuandikwa katiba mpya kunahaja gani ya marumbano ya hapa na pale,Ni kweli kabisa wote wanaoukataa mswada huo hauna kitu hata kimoja kinacho faa mpaka tukafikia hapa tulipo ?


Hata hivo Katiba ni kitu kinagusa maisha ya kila mtanzania kuna haja gani ya kuharakisha na kataa bila ya kuuchambua uliyopo nakuona mapungufu yake?.Tusiwe tunafuata mkumbo hata katiba yenyewe ilivyo andikwa hatuijui sawaswa.




No comments:

Post a Comment