Wednesday, April 13, 2011

DUNIANI KUNA MAMBO KWELI JAMANI TOKA LINI MAREHEMU ANAPOKEA MISHAHARA ?

Ukaguzi wa mahesabu ya fedha za serikali imebaini Halmashuri zetu zimejihusisha na malipo hewa.Malipo yaliyolipwa ni ya mishahara.Kinacho shangaza na haiingii akilini ya kumlipa mshahara marehemu.Inamana marehemu hao wanatoka kaburini kwenda benki kuchukua fedha?

Huwezi kuamini marehemu wa dizaini hiyo wanakwenda benki kukopa fedha,lakini mfanyakazi aliye hai akienda kuonana na meneja wa mikopo katika benki hizo hapati kwa urahisi,lakini marehemu wanapata mikopo hiyo kwa ulaini.

Lakini kila mwaka watumishi wa Umma wanajaza fomu za kuhakikisha au kuhakiki malipo ya mishahara hewa,inamana Halmashauri hizo zilizokubwa na ulipaji mishahara  hewa, huwa wanapeleka wapi fomu za uhakiki wa malipo hewa ya mishahara?

No comments:

Post a Comment