Monday, April 11, 2011

KAMATI KUU YA CCM NA SEKRETARIETI YAKE YAJIUZULU WHITE HOUSE DODOMA

Mwenye kiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho ushirikiano katika uongozi wa juu wa Chama hicho watakao chaguliwa,baada ya Kamati kuu na Sekretarieti kujiuzulu juzi usiku katika ukumbi wa White House jana.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa chama hicho kuwa na ushirikiano wa dhati na kamati kuu na Sekretarieti itakayo chaguliwa ili kuimarisha CCM.Alisema hayo baada ya uamuzi wa Kamati kuu  na Sekretarieti yake kujiuzulu katika uongozi wa juu kupisha wengine  wenye damu changa kuendeleza Chama.

Kamati kuu ya Chama Cha mapinduzi na Sekretarieti yake imejiuzulu jana katika mkutano wa NEC CCM, katika ukumbi wa White House mjini Dodoma jana.

Kati ya waliojiuzulu ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe.Yusufu Makamba kwa lengo la kuimarisha chama hicho.




No comments:

Post a Comment