Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani ( ILO ) Bwana Magunus Minja akitoa maelezo ya malengo ya Shirika hilo kwa usalama na afya kazini ili kuepusha ajali na vifo kwa wafanyakazi Duniani.
MAADHIMISHO ya siku ya Usalama na Afya kazini Kitaifa
yamefanyika katika uwanja wa Majimaji katika Manispaa ya Songea,Mgeni rasmi
alikuwa Waziri wa Kazi na Ajira Mheshimiwa Gaudensia Kabaka ,baada ya kufunga
maadhisho hayo alitoa zawadi katika taasisi 9 zilizo dhibiti viashiria vya
usalama katika kazini.
Mwakilishi wa Shirika la kazi Duniani Bwana
Magunusi Mijna alisema, Serikali ya Tanzania
leo imeungana na Shirika la Kazi Duniani (
ILO) waajiri,na awafanyakazi pamoja
na vyama vyao vinavyo simamia utamaduni wa usalama na afya sehemu za kazi,yenye
kauli mbiu “ Usimamizi wa usalama na
afya: Zana ya uboreshaji endelevu”
Bwa.Minja
alisema kuwa mwaka huu tunaadhimisha miaka 92
ya ILO kushughulikia haki katika jamii,kulinda maisha na afya ya wafanyakazi wote ikiwa ni
sehemu ya lengo pana la ILO la kazi yenye staha sehemu za kazi.
Alisema
kwa kunukuu kuwa “Kulingana na azimio la Seoul la mwaka 2008 kuwa utamaduni wa
taifa wa kulinda usalama na afya ni ule ambapo haki ya usalama na afya kazini
inaheshimiwa katika ngazi zote,ambapo serikali ,waajiri, na wafanyakazi
wanashiriki kikamilifu katika kufanikisha mazingira hayo.
Bw.Minja
alisisitiza kuwa kazi isiyo salama ni janga
la binadamu,ambayo husababisha
ajali,magonjwa na kupunguza uwezo wa kufanya kazi na kufupisha maisha ya
mfanyakazi.Ambapo kila mwaka mamilioni ya majanga hutokea bilia kuripotiwa.
Aidha alisema ili mfanya kazi awe salama
mahali pa kazi ni budi kufuata mifumo ya ( OSHMS
),kwa kuzingatia na kuandaa Sera ya
taifa ya usalama kazini na kuweka
miundombinu ya utekelezaji wa Sera na Programu zilizoandaliwa ,Programu ya
taifa ya usalama na afya kazini kwa kuwa na
malengo ya kitaifa kwa muda uliyo pangwa.
Alisema
ingawa ajali haina kinga lakini tahadhari ni muhimu kuchukuliwa na mfanyakazi
mwenyewe panapo tokea viashiria vya hatari sehemu ya kazi,kutoa elimu na
mafunzo ana kuzingatia sheria zilizowekwa na
Serikali, vyama vya wafanyakazi,waajiri
wafanyakazi na mashirika ya kijamii,ili kazi isiwe ya kufupisha maisha bali
iwaongezee maisha wafayakazi.