I wish you all the best to the coming new year of 2011,God will bless you and your lovely friends.
Friday, December 31, 2010
Sunday, December 26, 2010
JUMAPILI YA FAMILIA TAKATIFU ILIKUWA KAMA HIVI LEO KETU
Mr & Mrs Christian Sikapundwa baada ya kutoka kwenye ibada ya Christmas nyumbani kwao Dodoma
Familia ya Sikapundwa wakiwa nyumbani kwao wakipata chakula ikiwa ni ukamilishaji wa sikukuu ya Christmas
Kaka yake Mkubwa Bw.Sikapundwa Mzee Ally wa Kimamba Kilosa wakiwa katika kusheherekea Christmas.
waumini wa Kanisa la makole Manispaa ya Dodoma wakiangalia pango alipozaliwa Yesu Kristu katika zizi la wanyama.
Familia ya Sikapundwa baada ya chakula cha Christmas nyumbani kwao Uhindini,karibu na Makole Mjini Dodoma.
Familia ya Sikapundwa wakiwa nyumbani kwao wakipata chakula ikiwa ni ukamilishaji wa sikukuu ya Christmas
Kaka yake Mkubwa Bw.Sikapundwa Mzee Ally wa Kimamba Kilosa wakiwa katika kusheherekea Christmas.
waumini wa Kanisa la makole Manispaa ya Dodoma wakiangalia pango alipozaliwa Yesu Kristu katika zizi la wanyama.
Familia ya Sikapundwa baada ya chakula cha Christmas nyumbani kwao Uhindini,karibu na Makole Mjini Dodoma.
HERI YA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA KWA WATU WOTE ,PAMOJA NA FAMILIA TAKATIFU LEO
Hilo pango ni kiwakilishi cha eneo la zizi la wanyama ambapo Yesu Kristu alizaliwa mahali duni,ili kutimaza ahadi ya kumkomboa mwanadamu
Baaada ya ibada ya mkesha wa Christma,waumini wakionekana wakitoka katika ibada ya kwanza katika kanisa la Parokia ya Makole katika manispaa ya Dodoma.
Hiyo ni kwaya ya ibada ya asubuhi iliyo imba katika misa hiyo Christmas katika kanisa la Parokia ya Makole Mjini Dodoma.
Baaada ya ibada ya mkesha wa Christma,waumini wakionekana wakitoka katika ibada ya kwanza katika kanisa la Parokia ya Makole katika manispaa ya Dodoma.
Hiyo ni kwaya ya ibada ya asubuhi iliyo imba katika misa hiyo Christmas katika kanisa la Parokia ya Makole Mjini Dodoma.
Saturday, December 25, 2010
MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR OF 2011
The Rural Press staff wishes the all Bolger's readers merry Christmas and a happy beginning of new year 2011.And God will bless you and your family.
Thursday, December 23, 2010
MHESHIMIWA DIWANI MFAMAJI KUPITIA CHADEMA KATA YA MISUFINI AMEPATA SINTAFAHAMU PALE OFISI YAKE ILIPO CHOMWA MOTO NA WATU WASIOJULIKANA
Diwani wa kata ya Misufini katika Manispaa ya Songea Bw. Mfamaji amejikuta katika hali ya sintafahamu pale alipo kuta ofisi yake ikiteketea kwa moto,pamoja na nyaraka zake muhimu za kufasnyia kazi.
kwa mujibu wa watu walioshuhudia ofisi hiyo ikiteketea kwa moto na kujaribu kuisalimisha na kushindikana,walisema chanzo cha moto huo bado hakijajulikana,bali watu wasiojulikana ndio waliosababisha moto huo.labda kwa chuki zao zilizo wafanya kutimiza tendo hiho la fedhea,katika jamii yenye watu wenye akili wanaokubali ushindani ni kitugani.
Tuesday, December 21, 2010
POLISI WATEMBEZA MKONG'OTO NA MABOMU YA MACHOZI WA WASOMI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UNIVERSITY OF DODOMA ) UDOM KWA MADAI YA FEDHA ZA FIELD
hayo ni baadhi ya majengo yaliyojengwa ya Chuo Kikuu cha Dodoma kulingana vitivo mbalimbali
Uzuri wa majengo pekee haumtoshelezi mwanafunzi kufanya vyema katika masomo yake ya miaka mitatu au mnne na zaidi iwapo hatapatiwa mahitaji muhimu ya kufanikisha maendeleo ya masomo yake ikiwepo,research,pamoja na field mbalimbali .Iwapo hatapata mahitaji hayo wakati akiwa katika harakati za kutafuta shahada yake ndipo uzalendo unaondolewa na migomo inatawala ndani ya vyuo vyetu
Majengo ya Kitivo cha Social Science ambapo wanafunzi wa kitivo hicho jana walipata mkong'oto na kumwagiwa mabomu ya machozi,baada ya kugoma,wakiwa na madai ya fedha za Field zao,baadhi yao wamejeruhiwa na kulazwa hospitali ya Mkoa,hata hivyo wanadai kupeleka malalamiko yao kwa Waziri Mkuu.
Uzuri wa majengo pekee haumtoshelezi mwanafunzi kufanya vyema katika masomo yake ya miaka mitatu au mnne na zaidi iwapo hatapatiwa mahitaji muhimu ya kufanikisha maendeleo ya masomo yake ikiwepo,research,pamoja na field mbalimbali .Iwapo hatapata mahitaji hayo wakati akiwa katika harakati za kutafuta shahada yake ndipo uzalendo unaondolewa na migomo inatawala ndani ya vyuo vyetu
Majengo ya Kitivo cha Social Science ambapo wanafunzi wa kitivo hicho jana walipata mkong'oto na kumwagiwa mabomu ya machozi,baada ya kugoma,wakiwa na madai ya fedha za Field zao,baadhi yao wamejeruhiwa na kulazwa hospitali ya Mkoa,hata hivyo wanadai kupeleka malalamiko yao kwa Waziri Mkuu.
Saturday, December 18, 2010
JUMAMOSI YA LEO NAKULETEA MUENDELEZO WA MAKAO MAKUU DODOMA,NIKIANZAIA NA ROUND ABOUT TAMISEMI STAND YA DALADALA NA MAENEO MUHIMU KATIKA MANISPAA YA DODOMA
Round about ( TAMISEMI) katika Manispaa ya Dodoma
Stand ya daladala Jamatin ziendazo na zitokazo Mnadani ,Kuhungu,maili mbili
Jengo la NMB Dodoma pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDO),mtaa ambao ni maarufu sana uendao katika makao makuu ya CCM Mjini hapa.
Nyerere Square ambapo watu hupenda kupigia picha kwa ajili ya kumbukumbu kama alivyo mwanachuo wa CBE Bwana Joseph Sikapundwa katika bustani hiyo hivi karibuni.
Stand ya daladala Jamatin ziendazo na zitokazo Mnadani ,Kuhungu,maili mbili
Jengo la NMB Dodoma pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDO),mtaa ambao ni maarufu sana uendao katika makao makuu ya CCM Mjini hapa.
Nyerere Square ambapo watu hupenda kupigia picha kwa ajili ya kumbukumbu kama alivyo mwanachuo wa CBE Bwana Joseph Sikapundwa katika bustani hiyo hivi karibuni.
Thursday, December 16, 2010
Je unaijua Nyerere Square ,Manispaa ya Dodoma? Au Makao Makuu .
Nyerere square ni bustani iliyopo katika Manispaa ya Dodoma,imejengwa hapo kwa ajili ya kumbukumbu ya Baba wa taifa Mwalimu Julius Kambalage Nyerere katika makao Makuu ya Nchi.
Eneo hili watu hufika kupiga picha za kumbukumbu mbalimbali .
Pia kuna miti ya kivuli watu hupumzika na kujipatia vivywaji baridi,siku za kazi lakini siku za Juma mosi na Jumapili mgahawa huo haufanyi kazi,kumbe siku kama hizo ndiyo za kutangeneza fedha.Lakini usijali hayo karibu katika eneo hili la ukumbusho.
Eneo hili watu hufika kupiga picha za kumbukumbu mbalimbali .
Pia kuna miti ya kivuli watu hupumzika na kujipatia vivywaji baridi,siku za kazi lakini siku za Juma mosi na Jumapili mgahawa huo haufanyi kazi,kumbe siku kama hizo ndiyo za kutangeneza fedha.Lakini usijali hayo karibu katika eneo hili la ukumbusho.
Sunday, December 12, 2010
KIPINDUPINDU CHA LIPUKA NKUUNGU NA MAJENGO MANISPAA YA DODOMA
I meripotiwa kuwa wagonjwa 14 wa kipindupindu kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu katika Manispaa ya Dodoma katika maeneo ya Nkuungu na majengo.
Kufuatia mvua zilizonyesha katika maeneo kadhaa mkoani hapo,uchafu na maji machafu na matunda yanayouzwa na kuliwa bila kuyaosha na kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka kujisaidia kumeletea mlipuko huo.
Taadhari limetolewa na uongozi wa mkoa,kuwa wananchi wanashuriwa kuepuka kula vitu vya baridi,kuondoa uchafu kwani kipindupindu kinatoletwa na kula kinyesi kinacho sambazwa na inzi,kila mmoja anashauriwa kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni.
Saturday, December 11, 2010
Do you know the use of ubuyu fruit this Saturday?
The mibuyu trees situated at Ruwaha Mbuyuni,at Morogoro and Iringa Region tanzania,such trees are available at Chamwino Dodoma Tanzania ( source Christian Sikapundwa )
Ubuyu is a fruit from Mbuyu tree, mbuyu is a big tree are available in central Zone especial Dodoma ,Singida, very few in Southern Zone in Lindi, Region, Morogoro and Iringa Tanzania Ruwaha Mbuyuni Area.
Ubuyu fruit is very popular this time due to the struggling of life. Most people in town they use ubuyu to produce Ice – cream ubuyu, and others produce Ubuyu juice. There for the area where ubuyu fruit is found please use those fruit to make money.
Not only Ice cream, and juice from ubuyu, but also you can mix different colours ,and sugar with ubuyu so that you can produce good mixture which is very sweet ubuyu seed and then put them into the plastic bags and sell them to the children and Adults . (See pictures of mbuyu trees}
Thursday, December 9, 2010
UHURU MIAKA 49,TUDUMISHE UZALENDO...WATOTO 700 WA HALAIKI,200 KUTOKA VISIWAVI NA 500 TANZANIA BARA WABURUDISHA WANANCHI
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete akipokea heshima kutoka kwenye gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi,Polisi ,magereza na JKT katika uwanja wa Taifa siku ya maazimisho ya miaka 49 ya Uhuru jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akipungia wananchi katika uwanja wa Taifa leo siku ya kuazimisha miaka 49 ya Uhuru
Baadhi ya watoto 700 wa halaiki wakionyesha michezo ya sarakasi siku ya maazimisho ya miaka 49 ya uhuru.( MOTO: MIAKA 49 YA UHURU.TUDUMISHE UZALENDO.Jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Kikwete akipungia wananchi katika uwanja wa Taifa leo siku ya kuazimisha miaka 49 ya Uhuru
Baadhi ya watoto 700 wa halaiki wakionyesha michezo ya sarakasi siku ya maazimisho ya miaka 49 ya uhuru.( MOTO: MIAKA 49 YA UHURU.TUDUMISHE UZALENDO.Jijini Dar es salaam.
Monday, December 6, 2010
kipindupindu chaua wanne,watatu wa familia moja Manispaa ya Morogoro
Ugongwa wa kipindupindu sasa cha hamia manispaa ya Morogoro baada ya kuibuka katika Wilaya ya Mvomero,imeripotiwa kuwa wagonjwa 10 wamelazwa katika hospitali ya Mkoa wa Morogoro,na watu wanne wamefariki,kati yao watatu kutoka katika familia moja.
FURAHA YA WAZAZI NI KIJANA WAO KUPATA FAMILIA YAKE,MAMA WA MICAHEIL SIKAPUNDWA WAKIWA NA MJUKUU WAKE VERONICA
Mtoto Vero anapenda kurushwa rushwa,aona anavyo furahia kurushwa na Bibi yake Bibi Editha Sikapundwa mara baada ya kukaribishwa nyumbani kwao baada ya kutoka Dodoma, ambako alizaliwa tarehe 12/10/2010 katika Hospitali ya Mkoa huo,wakiwa kama wazazi wa Mikael na mkewe wanaungana nao katika kumshukuru Mungu katika kufanikisha maisha yao na hatimaye kupata mtoto.Walisema asante Mungu kwa yote mema yaliyopatikana.
SHUKURANI KWA MUNGU
Familia ya Bwana na Bibi Michael Sikapundwa wanamshukuru Mungu kwa ajili ya Mtoto wao mpendwa Baby Veronica Michael leo kutimiza mwezi mmoja na siku 26 tangu azaliwe tarehe 12/10/2010 katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma,ambapo sasa wapo nyumbani kwao Morogoro.
Saturday, December 4, 2010
RUVUMA YA FAULISHA KWA ASILIMIA 47.98 NA KUSHUKA KWA ASILIMIA 8.02 YA MWAKA JANA
Mshauri wa Elimu Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo akisoma taarifa ya maendeleo ya Elimu katika kikao cha Ushauri RCC katika ukumbi wa Songea Club hivi karibuni.
Aidha alisema kuwa waliochaguliwa bweni ni wanafunzi ni 103,ambapo wenye vipaji ni 31 wavulana 17 na wasichana 14,wanaokwenda ufundi ni 30 wavulana 27 na wasichana 3.Na waliochaguliwa kutwa ni 14,689 wavulana 7,469 na wasichana 7,220.
MKOA wa Ruvuma imefaulisha kwa asilimia 47.98,ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka huu,ikiwa imeshuka kwa asilimia 8.02 kwa matokeo ya mtihani wa taifa uliyofanyika mwaka 2009.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mshauri wa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo,mbele ya Kaimu katibu Tawala wa Mkoa huo,alisema wanafunzi 30,829 mkiwemo wavulana 14,986 na wasichana 15,843 waliofanya mtihani huo mwaka huu,kati yao 14,792 mkiwemo wavulana 7,537 na wasichana 7,255 ndio walio faulu sawa na asilimia 47.98. Ambao wataingia kidato cha kwanza mwakani.
Tuesday, November 30, 2010
IKIWA LEO NI MAADHIMISHO YA UKIMWI DUNIANI LAKINI UKIMWI BADO NI TATIZO KATIKA JAMII ZETU,KILA MMOJA WETU ACHUKUE TAHADHARI - MNJAGILA
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Nje ya Mfumo Rasmii Bwana Salum Mnjagila akitia saini kitabu cha wageni katika ofisi ya Afisa Elimu Wa Halmashauri ya Songea Vijijini Mkoani Ruvuma mwaka huu wakati wa ziara ya kukagua vituo vya MUKEJA na VICOBA Simanjiro,Njombe,Songea,Na Mahenge.( picha na Christian Sikapundwa )
Bwana Mnjagila pamoja na kukagua maendeleo ya vituo hivyo lakini hakusita kutoa tahadhari yuu ya VVU na UKIMWI katika jamii za watanzania.Alisema wanapojifunza jinsi ya kuzalisha mali katika ufugaji,ususi biashara ndogondogo na uwekaji wa akiba benki ,lakini pia wajifunze namna ya kuacha mambo yanayochangia maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa kuwa na mpenzi mmoja,kauacha mambo hayo au kutumia kinga.Hata kusikiliza ushauri wa wataalamu wa afya na ushauri wa viongozi wa Dini.
wakati leo ni maadhimisho ya UKIMWI Duniani Ruvuma wapo chini ya 33% ya upimaji wa hiyari
KAIMU Mratibu wa UKIMWI Mkoani Ruvuma Dkt Luitrid Komba asema changa moto bado ni kubwa kwa watu kujitokeza kupima afya zao kwa hiyari mkoani Ruvuma.Atoa wito kuwa watu wakapime afya zao,dawa za kurefusha maisha zinapatikana katika vituo vinavyo husika.
Wakati leo ni siku ya maazimisho ya UKIMWI Duniani mkoa wa Ruvuma ina asilimia 6.3 kutokana na taarifa ya watu waliojitokeza kupima afya zao Januari hadi Septemba mwaka huu.
Kaimu Mratibu wa UKIMWI mkoa wa Ruvuma Dkt.Luitfrid Komba alitoa taarifa hizo kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa RCC kilichofanyika Songea Club Novemba mwaka huu.
Dkt Komba alisema upimaji wa hiyari UKIMWI ni asilimia chini ya asilimia 33 kimkoa na kiwango cha watoto walioambukizwa ni asilimia 4.6.Aidha vituo 90 vinatoa huduma ya mama na mtoto ya kinga ya maambukizi ya UKIMWI.
Monday, November 29, 2010
Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya akemea vitendeo vya Wizi wa Ruzuku za Pembejeo
'Sikubali wala sinataruhusu Ruzuku za pembejeo zilizotolewa na serikali kuliwa na wajanja wachache wenye lengo la kuchukua vocha za mbolea na mbegu wakati mashamba hawana ili wakauze wapate fedha,sintavumilia kwa vitendo vya kuhujumu fedha za serikali.' Alisisitiza mkuu wa wilaya huyo kwenye kikao cha maendeleo cha mkoa ( RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Songea club.
Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya ambaye ni mwenye kiti wa Pembejeo za Ruzuku wilaya ya Songea,ndiye aliyeanzisha utaratibu wa barua za utambulisho wa shamba kwa wakazi wa mjini ili kulinda fedha za Serikali zisiliwe na wajanja wachache ambao hujifanya wana mashamba kumbe wanalengo la kuiba fedha za serikali kupitia Ruzuku za pembejeo,kitendo ambacho kinamkera Mkuu wa wilaya hiyo.
Aidha Bw.Sabaya amekemea kwa nguvu zote vitendo vivyosadikiwa vinafanywa na baadhi ya Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa vijijini na Vitongoji kutoza fedha kati ya shilingi 1,000/= hadi 5,000/= ili kuwapitishia barua hizo kuwa ni kero na ni dalili za rushwa na wakibainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu,(Source Juma Nyumayo)
PONGEZI
Mwenye kiti wa Ruvuma Press Bwana Juma Nyumayo kulia aliyevaa vuti akiwa na Makamu wake wa Press hiyo Bwana Mhidini Ndolanga aliyevaatai na Mjumbe wa Press hiyo Bi.Editha Karlo wa katikati akiwa akipata chai siku ya kikao cha kamati ya Maendeleo ya mkoa wa Ruvuma hivi karibuni Songea Club ( Picha Na Christian Sikapundwa )
Chama cha Waandishi wa Habari Mkoani Ruvuma (RPC) kinawapongeza viongozi waliochaguliwa wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Kilimanjaro ( MECK ) kwa kuaminika na wanachama wao na kuwapa ofisi yao ambayo ni mdau mkubwa wa maendeleo.
Mwenyekiti wa Ruvuma press club Bwana Juma Nyumayo,amesema kamati ya muda chini ya uongozi wa mwenyekiti Josephine Sanga,ilifanya kazi nzuri na kuweka misingi imara kufikia uchaguzi wa Kidemokrasia uliowachagua viongozi wapya.
Hongera sana endeleeni kushirikiana kwa maendeleo ya Kilimanjaro,Kanda ya Kaskazini na Taifa zima kwa ujumla ( Source Juma Nyumayo ).
HICHO NDICHO KILICHO PIGIWA KELELE NA WAJUMBE WA BOARD YA BARABARA MKOANI RUVUMA KWA MKUU WA MKOA DKT CHRISTINE ISHENGOMA
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt Ishengoma allisema fedha za serikali za ujenzi wa barabara zitumike kwa kujenga barabara zenye viwango vilivyo bora katika kikao cha bodi ya barabara kilicho fanyika katika ukumbi wa Songea Club,Alikuwa sahihi.Je hiyo barabara ya kiwango cha lami katikati mji wa Manispaa ya Songea itokayo CCM Wilaya kuelekea kanisa la Anglikana ilijengwa kwa viwango vya ubora unaotakiwa ? .( picha na Christian Sikapundwa )
FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA ZITUMIKE KWA UJENZI ULIO BORA WA BARABARA ZETU - DKT ISHENGOMA
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt Christine Ishengoma katika kikao cha Board ya barabara Songea Club tarehe 26/11/2010
MKUU wa mkoa wa Ruvuma Dkt Christine Ishengoma amekemea tabia ya baadhi ya Halmashauri mkoani hapa kutumia fedha za ujenzi wa barabara visivyo hasa kujenga vipande virefu bila ubora. ‘Afadhali mjenge barabara km moja ( 1 ) yenye ubora kuliko km 4 kwa fedha hiyo bila ubora.’Alishauri Dkt Ishengoma.
Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara mkoani Ruvuma kilichoketi tarehe 26/11/2010 Songea Club walipeleka masikitiko yao makubwa kwa halmashauri ya Manispaa ya Songea. Kwa ujenzi wa barabara na matengenezo bila viwango.
Hata hivyo waliipongeza,Halmashauri ya Mbinga katika ujenzi wa barabara za kiwango cha lami pia wakala wa Barabara mkoani TANROADs kusimamia vyema mitandao na kujenga barabara na madaraja.( Source Juma Nyumayo )
Sunday, November 28, 2010
Siku 16 za kupinga ukatili za kijinsia Tanzania,wanaharakati,jamii isilifumie macho jambo hilo
Siku 16 za maandalizi ya kupinga ukatili wa kijinsia miongoni mwa watanzani,unafanyika kikanda kama ilivyo ainishwa na wanaharakati wa kupinga unyanyasaji wa kijinsia katika jamii zetu za kitanzania.Hasa kufuatia mila na desturi za kiafrika kuwa na mfumo dume,mfumo boss,na hata mfumo jike.Dkt Judith Tudunga alisema kupitia vyombo vya habari kuwa ukatili wa kijinsia umetawala sana katika jamii zetu.
Wito wake kwa watanzania kuwa wakisikia jirani anapigwa ama kufanyiwa vitendo ambavyo vinamdharirisha wajitokeze kwenda kutoa msaada.Alisema unyanyasaji na ukatili wanaofanyiwa baadhi ya tanzania unasaidia kurudisha nyuma maendeleo ya ,mtu binafsi na hata Taifa zima kwa ujumla.
Saturday, November 27, 2010
WABUNGE WA CHADEMA WALISUSIA HOTUBA YA RAIS KIKWETE BUNGENI KWA KUTORIDHISHWA NA MATOKEO YA KURA ZA URAIS
Mhe.Freeman Mbowe katika mdahalo wa kambi mbili ndani ya Bunge la 10 linatoa picha gani kwa wapigakura wao uliofanyika Jijini Dar es salaam Jumamosi ( Picha na Christian Sikapundwa }
Kiongozi wa Kambi ya upinzani katika Bunge la 10 Mhe.Freeman Mbowe alisema kutoka katika Bunge wakati Rais kikwete akifungua Bunge la 10 Mjini Dodoma hivi karibuni, wabunge wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ni kuwakilisha kilio chao mbele ya Rais,Wabunge wa vyama vingine na Chama Tawala pamoja na wanachi kuwa kitendo cha Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Urais katika baadhi ya majimbo si mzuri.Ufanyiwe marekebisho.
Aidha alisema kuwa wao hawajsema kuwa hawamtambui Rais Kikwete,bali kilio chao ni matokeo ya uchaguzi yalikuwa na kasoro,na alisema wataendelea kushirikiana na wabunge wote ili kuleta mustabali wa kumletea mwananchi maendeleo ambao ni wapiga kura wao.
IJUMAA NA JUMAMOSI LEO MSIMU WA MVUA UMEANZA KWA RASHA RASHA MJINI SONGEA
Kumbe watu hawaogopi magari bali mvua huwa wanatimua mbio za ajabu kwenda kujificha wasilowane,nimeshuudia mwenyewe pale mvua ilipo nyesha kwa mshitukizo hapo jana na leo katika Manispaa ya Songea,waenda kwa miguu kivyao,waendesha baiskeli vivyo hivyo na wenye pikipiki na wateja wao basi maradi patashika.
Lakini pamoja na hayo hizo ni ishara kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kuanza kuandaa mashamba yao kwa mazao ya chakula ambayo ni mahindi, msimu uliyopita mkoa huo umezalisha mahindi mengi kuliko msimu wowote wa kilimo cha mahindi,Ruzuku za pembejeo zimesha fika kwa mbolea na mbegu kwa msimu huu wa kilimo.
Friday, November 26, 2010
WHEN WOMEN WILL BE FREE FROM SEXUAL VIOLENCE IN SOME OF THE AFRICAN COUNTRIES?
Margot Wallstrom is fighting against sexual violence in women in African Country through International violence against women in Africa.she is U.N.Special Representative for this matter.
Kenya,Congo DRC,Zimbabwe, Rwanda and Burudi women are reported to be the victims of sexual violence by Armies, some are raped and killed, women are suffered unfortunately, a girl may raped by ten boys at a time.
In Zimbabwe rape are used as a weapon of war, some kind of tact ticks to use women to torture them which affect the women psychologically and mentally.
The one on one with Maargot Wallstrom U.N. Specially representative on sexual violence had said that sexual violence against women in Kenya more than one women a week was reported killed by her male partner.
Also in Zimbabwe five women a week were murdered by a male partner or family member this situation will continue until when, no peace in women at all in some of African Continent.
The great percentage pf women in Africa suffer from this violence especial in rural areas where they are not adequately educated.
And some even go through this violence and choose to remain silent about it because of the fear of being stigmatized by the member of their community.
What is your comment about this sexual violence against women in Africa exercised by armies, drug user and what the International violence against woman you want to act about this matter?
But Betty Makoni in Zimbabwe reported that poverty in women in that Country is the main problem for them to be raped and other violence against many women. ‘ Women and men are not equally in African Country because a lot of them are victimized by men.’ She said.
INDIGO AVIATION FLY TO SONGEA ANY TIME FROM NOW
The Air port manager of Songea Airport Mr.Valentine Fasha explain to the members of RCC Ruvuma in Songea Club yesterday how the INDIGO AVIATION Plane will work and how process will be taken before to start it's journey.
The Airport manager of Songea Airport Mr.Valentine Fasha told the members of RCC meting held at Songea Club yesterday that the Indigo Aviation is not a new in Tanzania,but it’s now routing Dar es salaam to Pemba.’Also it is a big plane caring 25 to 30 passengers at a time’. Said Mr Fasha.
The Hon.DR.Christine Ishengoma Regional Commissioner of Ruvuma comment on the Indigo Aviation to start it’s route to Songea, because it will simplify the bus journey which take longer time to reach Dar es salaam.
Moreover the business man of any level, officials figures and other people will benefit with that airway journey. And she told Mr.Fash to introduce the man to her how want to start airway journey from Songea to Dar es salaam as soon as possible.
MHE.DKT.CHRISTINE ISHENGOMA AKERWA NA WAHARIBIFU WA MAZINGIRA MKOANI RUVUMA
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt.Christine Ishengoma akiongea na wadau wa maendeleo mkoani wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa ( RCC ) katika ukumbi wa Songea Club naja ( Source Christian Sikapundwa ).
MKUU wa Mkoa wa Rvuma anakerwa na watu wanaochangia uharibifu wa mazingira katika mkowa wa Ruvuma kwa kuchoma mkaa,kukata miti bila kupanda mingine,kuchoma misitu bila sababu,kitendeo ambacho kitakaribisha ukosefu wa mvua na hatimaye kuwepo kwa jangwa.
Mkuu wa mkoa huo alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC ) katika ukumbi wa Songea Club,ambapo aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapo kuzingatia kanuni za kuhifadhi mazingira na kuyatunza,na wachoma mkaa wapewe vibali vya kufanya shughuli hizo.
Dkt.Ishengoma alisema utekelezaji wa miradi ya Millenia ( millennium Challenge ) umeanza kuanzaia Jun mwaka huu kwa kuanza na ujenzi wa barabara kwa viwango vya lami.Songea hadi Namtumbo kilometa 67 kwa mkataba wa miezi 27 ambao utaishia September 2012.
Nyingine ni Barabara ya Peramiho hadi Mbinga inayojengwa na kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd amekabidhiwa mradi huo mwezi Agasti mwaka huu kwa mkataba wa miezi 27 na atakabidhi mradi huo mwezi Oktoba mwaka 2012.
Aidha Dkt Ishengoma alisema uchangiaji wa maoni,ushauri wa wajumbe wa kikao hicho kinachangia maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa kiwango cha juu,alisema mkoa unaendelea kujitosheleza kwa mazao ya chakula na kuzalisha ziada kwa ajili ya kuuza ndani na Nje ya mkoa.
Alisema wananchi wasiuze mahindi yote bali waache mahindi mengine kwa ajili ya chakula chao na familia zao,alisema uzalishaji umeongezeka kutoka tani 652,462 msimu wa 2008/2009 hadi tani 1,127,589 msimu wa kilimo wa 2009/2010 sawa na asilimia 72.8.
Alisema mkoa umelenga kuzalisha tani 107,882 za mazao ya chakula na tani 1,149,164 za mazao ya biashara na amewapongeza wakulima wote kwa ujumla wao wa mkoa huo kwa kuzalisha mazao ya chakula na biashara ingawa kulikuwa na mapungufu ya kitaalamu yalijitokeza katika kilimo musimu uliyopita.
Pia alisema Serikali imeshatoa shilingi 12,809.000.000/= za kununulia mahindi hadi sasa tani 37,090.4 zenye thamani ya shilingi 11,,410,010,460/= na ununuzi unaendelea,alisema mkoa umepokea Vocha 518,060 za Ruzuku ya pembejeo zenye thamani ya shilingi 10,781,360,000/= zitakazo nufaisha wakulima 172,900 kwa musimu wa kilimo uliyopita.
Katika musimu huu wa kilimo wakulima 203.412 sawa na ongezeko la asilimia 17.9 watanufaika na ruzuku ya pembejeo,ambapo Wizara imetoa Vocha za mbolea ya kupandia 203,412 zenye thamani ya shilingi 5,288,712,000/= na vocha za mbegu 203,412 zenye thamani ya shilingi 4,041,040,000/=
Wednesday, November 24, 2010
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEUA BARAZA LA TATU LA MAWAZIRI LEO KATIKA AWAMU YAKE YA KUIONGOZA NCHI KUPITIA CCM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu ya Jijini Dar es salaam ameteua Baraza lake la Mawaziri,likiwa ni baraza la tatu tangu aingie madarakani.Baraza la kwanaza lilikuwa mwaka 2005 la pili mwaka 2008 na la tatu mwaka 2010.Hongera kwa uteuzi wake ni matumaini ya watanzania kuwa ameteua watu wachapa kazi kwa umahiri wa hali ya juu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi ni Mheshimiwa Shukuru kawambwa,ambapo Waziri wa Elimu wa awali Prf .Jumanne Maghembe amepelekwa Wizara ya Kilimo na Chakula.
Saturday, November 20, 2010
JIAJIRI KUPITIA UFUNDI PIKIPIKI MWONE JOHN JOHN KOMBA SODECO SONGEA
Fundi pikipiki Bw.John John Komba akiwa dukani kwake,ukihitajika spare ya pikipiki hakuna haja ya kwenda kununua kwa mwenzake.
Fundi John Komba akimwelekeza mwanafunzi wake wa mwaka wa pili Bw.Emelian Mbepela kufunga taa za pikipiki aina ya SANLG,ni aina za pikipiki zilizoko kipindi hiki,aina ya SUZUKI kwa mwanafunzi kama huyu itakuwa shida kwake.
Fundi John Komba akimwelekeza mwanafunzi wake wa mwaka wa pili Bw.Emelian Mbepela kufunga taa za pikipiki aina ya SANLG,ni aina za pikipiki zilizoko kipindi hiki,aina ya SUZUKI kwa mwanafunzi kama huyu itakuwa shida kwake.
UFUNDI wa kutengeneza pikipiki Katika Manispaa ya Songea umesaidia sana vijana wengi kujiajiri baada ya kupata mafunzo hayo kwa miaka miwili tu,kisha kwenda kufungua gereji zao mitaani,ndani ya Manispaa au nje ya manispaa hiyo.
Fundi pikipiki katika maeneo ya SODECO katika Manispaa ya Songea Bwana John John Komba alibainsha hayo kwenye gereji yake kuwa alianza kujiunga katika fani hiyo mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1988.
Alisema kuanzia mwaka 1988 aliafungua gereji yake Mahenge katika manispaa hiyo hiyo ambapo alianza kupokea vijana waliotaka kujifunza,kipindi kile kila kijana alilipa sh.50,000 tu lakini mabadiliko ya nyakati,kijana anatakiwa kulipa sh.200,000. Na mafunzo ni kwa miaka mitatu.
Aidha alisema tangu aanze kufundisha vijana hao ni zaidi ya 15 wapitia katika gereji yake,na wamekwisha jiajiri katika wilaya za Mbinga,Tunduru,Namtumbo na katika Manispaa ya Songea.kwa sasa ana wanafunzi wanne.
Kwa mzamzi yeyote mwenye mtoto anayehitaji kujiajiri kupitia ufundi pikipiki amwone Fundi JJ Komba,zaidi ya hayo ana duka la spare parts za pikipiki SODECO Songea Mkabala na Soko la kuuza mazao ya chakula.
Thursday, November 18, 2010
Wabunge wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa baraza la mawaziri watakaoteuliwa hapo baadaye
Rais Kikwete akitia saini baada ya kumwapisha waziri Mkuu Mizengo Pinda Ikulu ya Chamwino Dodoma leo na saa 10.30 alihutubia Bunge,ambapo waheshimiwa wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya Bunge hilo mbele yake kwa tishio la kususia hotuba yake.
Pamoja na hayo Rais aliendelea na hotuba yake na Wabunge wa CCM na Vyama vingine ya Upinzani waliokuwemo.Na kuweka kambi isiyo rasmi Bungeni humo
Pamoja na hayo Rais aliendelea na hotuba yake na Wabunge wa CCM na Vyama vingine ya Upinzani waliokuwemo.Na kuweka kambi isiyo rasmi Bungeni humo
RAIS Jakaya kikwete amewataka wabunge wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,kutoa ushirikiano wa kutosha kwa baraza la mawaziri watakao tuliwa baadaye,ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi wa kutosha.
Dokta Kikwete alisema hayo wakati alipoto hutuba yake ya kufungua Bunge la kumi la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ,mjini Dodoma leo na kutagaza vipaumbele vyake vya kuleta maendeleo vitakavyo tekelezwa ndani ya miaka mitano ijayo.
Alitaja baadhi ya vipaumbele hivyo ni pamoja na kusogeza huduma za afya kwa kuoboresha huduma zake,na kuongeza bajeti katika sekta ya afya,kuimarisha sekta ya madini,kuboresha miundo mbinu ya barabara, na reli,kuanzisha benki ya kilimo.
Vingine ni pamoja na kuimarisha sekta ya elimu kwa kuboresha mazingira
yakujifunzia na kufundishia na kutoa maslahi kwa walimu kujenga nyumba za walimu,kuimarisha sekta ya utalii ambayo ni ya pili kwa kuiingizia fedha za kigeni nchini.
Nyingine ni kumkomboa mwananchi kwa kuendeleza programu ya kilimo nchini,kwani mazo ya chakula na biashara yameongezeka kweli msimu huu,na kuimarisha sekta ya viwanda kwa kuendeleza viwanda,na kuimarisha sheria mpya ya kupambana na rushwa.
Kipaumbele kingine ni pamoja na kuendeleza vipaji vya wasanii,wa muziki,filamu,maigizo na kuimarisha michezo itakayo fundishwa shuleni,walimu wenye fani za michezo wafundishe michezo,na kuimarisha utoaji wa haki kwa wananchi.
Pia Dkt Kikwete alisistiza kuwa yeye ni Rais wa wote waliomchagua na wasio mchagua,wakiwa na matatizo watakwenda kwake kusema shida zao,ni Rais aliyechaguliwa na CCM na vyama vingine.
Aidha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda alitoa shukurani kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa maelekezo ya kutekelezwa baada ya kuteua baraza la mawziri, ambapo akiwa kiongozi mkuu wa serikali atatekeleza kwa kusaidiana na baraza la mawaziri na wabunge wote.
Mhe.Pinda alitoa angalizo kuhusu umoja wa watanzania kuwa usigeuzwe kuwa jambo dogo,wala asiruhusiwe mtu mmoja mmoja,kikundi cha watu au chama kuonyesha dalili ya uvunjifu wa amani nchini.
Alisema kuwa kuna baadhi ya vyama haviwa tii moyo hata kidogo wananchi,kwa hali hiyo si mwelekeo mzuri kwa nchi yenye amani na utulivu Tanzania,na kupongeza ukuzaji wa kipato cha mwananchi kwa kuendeleza sekta ya kilimo,ufugaji na uvuvi.
Alitoa ahadi kuwa ataekeleza magizo hayo kwani kila mbunge amaetoka kwa wananchi wenye vipato vinavyotegemea kilimo na kisha aliairisha Bunge hilo hadi tarehe 8/2/2011 saa 3.30 asubuhi.
Mheshiwa Mizengo Pinda apishwa kuwa Waziri mkuu wa Bunge la 10 Chamwino Ikulu Dodoma
Mheshimiwa Mizengo kayanza Pinda ( Mbunge ) wa Katavi apishwa kuwa waziri Mkuu wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chamwino Ikuli nje kidogo ya Manispaa ya Dodoma ,wakati wabunge wa Chama cha CHADEMA hawakuonekana katika sherehe hizo,Swali hawakualikwa,ama wametekeleza kauli ya aliyekuwa akitaka kiti cha Urais kushindwa Dkt Slaa Kutomtambua Kikwete kama ndivyo tuwaelewe vipi?.wewe na mimi tutafakkari,Je shughuli za kuapishwa waziri Mkuu hazikufanikiwa,na Rais Jakaya Kikwete hawezi kuhutubia Bunge la kumi la mwaka 2010 kwa kuwa wabunge wa CHADEMA wamesusia,Ni aibu kwa wapenda amani,pia ni mashaka kwa wale waliojenga imani kuwa ni chama kitakacho tawala nchi hapo baadaye.Lakini kama ilikuwa babahati yako ya kuwa Rais subira ni muhimu.Mheshimiwa Mizengo Pinda akila kiapo mbele ya Rais Jakaya Kikwete Chamwino Ikulu Dodoma Leo
Dkt Slaa kutomtambua Rais Kikwete kunazua maswali mengi miongoni mwa watanzania
Dkt Slaa wa CHADEMA katika Hekaheka za kutafuata Urais wa Tanzania 2010 ( Source Christian Sikapundwa)
KUFUATIA kauli ya Dkt Wilbroad Slaa ya kutomtambua Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete,kunazua maswali mengi kwa baadhi ya watanzania wenye akili sawasawa, wenye kujua asiyekubali kushindwa si mshindani.
Kwa mujibu wa kauli hiyo wabunge wa chama chake cha CHADEMA nao bila kujua, kwa makusudi, kuwa waliapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda kuwa watakuwa waaminifu, watailinda,wataitete katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumalizia kusema Mungu awasaidie.
Lakini cha ajabu haohao waliosema hivyo, kwa kufuata kauli ya Slaa asiyekubali kushindwa na kutomtambua Rais Kikwete,leo wamekataa kushiriki kuapishwa kwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma.
Zaidi ya hayo wanaendelea kuwa watasusia hotuba ya Mhe.Rais Kikwete, itakayo tolewa leo moja kwa moja na Vyombo vya habari, kufuatia kauli ya Rais wao Dkt Slaa, aliyeshindwa kuwa Rais halali wa nchi hii, hivyo wanataka wananchi na jamii ya kimataifa ambayo ilithibitishiwa na watazamaji wa ndani na nje wakiwemo TEMCO, SADC,EAC,EU, UN kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wahaki. CHADEMA wanataka kujenga Tanzania ya namna gani?.
Wananchi wanaanza kuwa na maswali mengi kufuatia uamuzi wa wabunge hao kati yao ni wasomi, hivyo hao wamesoma vyuo gani ambako hawakujifunza Saikolojia,Lojiki ya mambo yanavyo kwenda katika ulimwengu huu.
Kuchaguliwa au kutochaguliwa ni matakwa ya yule atakaye kukuchagua au kutokuchagua,hivyo hayo hawayajui? au mradi kuuonyesha ulimwengu kuwa wao wanaweza kususia,hivyo ni wote walikubaliana au ni ‘msafala wa mamba na kenge nao wapo’.
Kama utafanikiwa kusoma Blog hii, jaribu kumrudia Mungu wako na kusema Eee Mungu nisamehe,na urudi Tanzania maana ninyi tunakuwa na mashaka nanyi,mnaelekea kubaya,wale wenzenu wamezoea,wamekulia katika hekeheka za kutengena na familia zao,kwetu ni jambo geni linahitaji maandalizi ya kutosha.
Watanzania hawajui, na hao wafuasi ambao wanawashabikia si lolote,hawana mbinu za kujihami,kutokana na hali zao zilivyo,tusipoteze amani na utulivu tuliouzoea, Baadhi ya nchi duniani zimekubaliana na matokeo uchaguzi 2010 na sheria,kanuni na taratibu zilizotawala uchaguzi huo zilifutwa ikiwa ni pamoja na kandaa uwanja sawa wa ushindani hapakuwa na malalamiko.
Hivyo hao waliosusia kuapishwa Waziri Mkuu Pinda,na baadaye kususia hotuba ya Rais Bungeni hapo baadaye,wataingia tena katika Mjengo wa Bunge? kuendelea na vikao vyake,wenyewe wanajionjaje kwa wenzao? Wabunge wenzao wa chama Tawala CCM na kambi vyingine za upinzani ambao si CHADEMA nao wanawaonaje? Jamii ya watanzania wanawaonaje? bado watakuwa na imani na chama hicho ( CHADEMA )
Tuesday, November 16, 2010
WAZIRI MKUU MIZENGO KAYANZA PETER PINDA ATHIBITISHWA KWA KURA 277 SAWA NA ASILIMIA 84.5 ZILIZOPIGWA NA WABUNGE WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda mbunge wa Jimbo la katavi amethibitishwa kwa Waziri Mkuu kwa kupigiwa kura na wabunge 328,ambapo kura zilizoharibika ni 2 sawa na asilimia 0.6,waliosema hapana 49 sawa na asilimia 4.9 na waliosema ndio ni 277 sawa na asilimia 84.5
Baada ya kuthibitishwa kwake Mhe.Pinga alimshukuru Mungu ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,wahehsimiwa Wabunge kwa kuthibitisha kuwa Waziri Mkuu,aidha alisema kuwa atakuwa Waziri mkuu wa wabunge wote,waliomkataa na waliomkubali kwa lengo la kumsaidia mwananchi.
Alisema kuwa kweli yeye ni mtoto wa mkulima hivyo ameomba ushirikiano mkubwa na wabunge wote wakulenga mkulima,mfugaji,mvuvi na mrina asali,hata kukiwa na malumbano lakini yawe yana lenga kumtetea mwananchi mkulima.
Saturday, November 13, 2010
MKOA WA RUVUMA WAPOTEZA MRATIBU WA KIFUA KIKUU NA UKOMA BWANA RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU KWA TATIZO LA KISUKARI NA MOYO
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA MRATIBU WA KIFUA KIKUKU NA UKOMA HOSPITAL YA MKOA WA RUVUMA ALIYEFARIKI TAREHE 12/11/2010 SAA 9 ALASIRI.
Alizaliwa tarehe 01/3/1952 Kidodi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro,akapata elimu ya msingi Lumango Luhembe kidodi.Hatimaye alipata elimu ya Sekondari nchini Uganda kidato cha kwanza hadi cha tatu,machafuko ya kisiasa yalivyoanza nchini Uganda ,Marehemu alirudi Tanzania .
Alivyorudi Tanzania alijiunga na chuo cha waganga wasaidizi ( watabibu ) Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro,baada ya mafunzo hayo alipelekwa kuanza kazi ya ugnaga Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 1976 ambapo alifanya kazi kwa muda mfupi.
Mwaka 1979 alihamishiwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambapo mwaka 1980 alikwenda kwa masomo ya stashahada chuo cha uganga Bumbuli Tanga mwaka 1982 alihitimu mafunzo yake na kurudi hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kama Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma hadi mwka 2006.
Mwaka alianza kupata tatizo la kisukari na moyo,ambapo tarehe 26/12/2006 tatizo likazidi kuwa kubwa na akaendelea kuugua hadi tarehe 12/11/2010 saa 9 alasiri Mratibu Mwikwa akafariki katika hospitali ya mkoa ya Songea,Na mazishi yatafanyika tarehe 15/11/2010 Mjimweme katika manispaa ya Songea,ambako familia yake inaishi hapo.Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa.
Atakumbukwa na watu wengi kwa utendaji wake wa kazi ambao haukuwa na mpaka,hakujali umbali wala unyanyapaa wa aina yoyote.Alikuwa mwepesi wa kutoa ushauri na kutoa msaada kwa wagonjwa wake,alikuwa mcheshi,mwingi wa tabasamu,na maneno ya kumtia mgonjwa faraja.Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.
Friday, November 12, 2010
SPIKA WA KWANZA MWANAMKE WA BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE.ANNE SHEMAMBA MAKINDA WA CCM ALIYE PATA KURA 265 SAWA NA ASILIMIA 74.2 AMEANZA KAZI YA KUAPISHA WA BUNGE MARA BAADA YA KUTANGAZWA KWAKE MJINI DODOMA LEO TAREHE 12/11/2010
Mheshimiwa Samwel John Sitta Spika aliyestaafu akimkimbatia Mhe. Anne Shemamba Makinda Spika wa CCM aliyechaguliwa na wabunge hao kwa kupata kura 265. sawa na asilimia 74.2 na kumshinda Mgombea wa nafasi hiyo Bwana Mabere Nyauchi Marando wa CHADEMA kwa kura 53 sawa na asilimia 16.2.Baada ya Mhe.Sitta kuaapa kuwa atahifadhi,atailinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Tanzania iliyowekwa..
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungaqno wa Tanzania aliyechaguliwa kushika nafasi hiyo Mhe. Anne Shemamba Makinda akipeana mikono na Mhe.John Momose Cheyo baada ya kuapa kuwa atakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Rashid Ally Abdalah akipeana mikono na Spika wa Bunge la 10 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Anne Shemamba Makinda baada ya kuchaguliwa kuwa Spika wa Bunge hilo na kuahidi kuwa ataendesha Bunge hilo kwa kanuni za Bunge zilizo wekwa kwa mujibu bila upendeleo.
Saturday, November 6, 2010
DOKTA JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEAPISHWA LEO KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO KWA KIPINDI CHA MIAKA MITANO IJAYO
Baada ya kuapishwa Rais na Makamu wa Rais waliombewa Duwa na madhehebu ya kidini ili kuwaombea waongoze kwa amani na utulivu.Kisha alikaribishwa kuwahutubia wananchi alisema hawezi kusema mengi,mengi atasema siku ya kuhutubua Bunge siku chache zijazo.
Ametoa shukurani kwa Mungu,na wananchi kuchagua CCM kwa kuona jinsi walivyo jiandaa kulitumikia taifa.Alisema watembeeni kifua mbele kwani watanazia bado wanaipenda CCM,pia alimshukuru Makamu wa Rais na mke wake kwa kumsaidia katika kufanikisha azima ya kuwa Rais.
Aidha alisema hakuweza kusahau viongozi wa vyama vya siasa vilivyotoa hamasa kubwa kwa CCM,Alisema uchaguzi umepita sasa watu wagange yajayo.Katika baadhi ya maeneo kulipandikizwa sumu mbaya ya kuwagawa watanzania aliomba yaachwe hayo.
Alisema watanzania wasiaharibu sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa lengo la kupata madaraka.pia aliwapongeza Tume ya Uchaguzi jinsi ilivyo fanikisha uchaguzi huu uluyopita,vyombo vya usalama na vyombo vya habari .
Ametoa shukurani kwa Mungu,na wananchi kuchagua CCM kwa kuona jinsi walivyo jiandaa kulitumikia taifa.Alisema watembeeni kifua mbele kwani watanazia bado wanaipenda CCM,pia alimshukuru Makamu wa Rais na mke wake kwa kumsaidia katika kufanikisha azima ya kuwa Rais.
Aidha alisema hakuweza kusahau viongozi wa vyama vya siasa vilivyotoa hamasa kubwa kwa CCM,Alisema uchaguzi umepita sasa watu wagange yajayo.Katika baadhi ya maeneo kulipandikizwa sumu mbaya ya kuwagawa watanzania aliomba yaachwe hayo.
Alisema watanzania wasiaharibu sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa lengo la kupata madaraka.pia aliwapongeza Tume ya Uchaguzi jinsi ilivyo fanikisha uchaguzi huu uluyopita,vyombo vya usalama na vyombo vya habari .
Friday, November 5, 2010
DOKTA JAKAYA KIKWETE ATANGAZWA KUWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BAADA YA KUPATA ASILIMIA 61.17
Dokta Jakaya Kikwete atangazwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kushinda kwa asilimia 61.17,akifuatiwa na Dokta Willbroad Slaa wa CHADEMA kwa asilimia 26.34 na hakufika kwenye matangazo hayo,ambapo mshidi wa tatu ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata asilimia 8,06.
Profesa Lipumba alimpongeza Dokta Kikwete kwa ushindi aliyoupata na kumpatia Ilani ya CUF isaidie kuleta Demokrasia nchini,katika ahadi kadhaa zilizo ahidiwa wakati wa kuwaomba wanachi ridhaa ya kuiongoza nchi.kama vile ajila kwa vijana,kuboresha elimu,miundombinu na ustawi wa jamii.
Dkt Kikwete kawashukuru watanzania wote kwa kuichagua CCM,Tume ya Uchaguzi,Vyombo vya habari kwa mchango wao,Wangalizi wa Uchaguzi,na kuwaeleza wananchi kuwa uchaguzi umepita kwa utulivu na Amani.
Profesa Lipumba alimpongeza Dokta Kikwete kwa ushindi aliyoupata na kumpatia Ilani ya CUF isaidie kuleta Demokrasia nchini,katika ahadi kadhaa zilizo ahidiwa wakati wa kuwaomba wanachi ridhaa ya kuiongoza nchi.kama vile ajila kwa vijana,kuboresha elimu,miundombinu na ustawi wa jamii.
Dkt Kikwete kawashukuru watanzania wote kwa kuichagua CCM,Tume ya Uchaguzi,Vyombo vya habari kwa mchango wao,Wangalizi wa Uchaguzi,na kuwaeleza wananchi kuwa uchaguzi umepita kwa utulivu na Amani.
Subscribe to:
Posts (Atom)