Saturday, November 27, 2010

IJUMAA NA JUMAMOSI LEO MSIMU WA MVUA UMEANZA KWA RASHA RASHA MJINI SONGEA

Kumbe watu hawaogopi magari bali mvua huwa wanatimua mbio za ajabu kwenda kujificha wasilowane,nimeshuudia mwenyewe pale  mvua ilipo nyesha kwa mshitukizo hapo jana na leo katika Manispaa ya Songea,waenda kwa miguu kivyao,waendesha baiskeli vivyo hivyo na wenye pikipiki na wateja wao basi maradi patashika.
Lakini pamoja na hayo hizo ni ishara kwa wakulima wa Mkoa wa Ruvuma kuanza kuandaa mashamba yao kwa mazao ya chakula ambayo ni mahindi, msimu uliyopita mkoa huo umezalisha mahindi mengi kuliko msimu wowote wa kilimo cha mahindi,Ruzuku za pembejeo zimesha fika kwa mbolea na mbegu kwa msimu huu wa kilimo.

No comments:

Post a Comment