Pamoja na kumaliza hekaheka za kampeni za Urais Ubunge na Udiwani ikaingia ngwe nyingine ya upigaji wa kura tarehe 31.10.31 2010 ulikamilika kwa Amani na Utulivu mkubwa,wananchi walitimiza haki yao ya msingi kumchagua kiongozi wanaye mtaka.
Ikaingia hatua ya mwisho ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo,ambapo vyama vyilivyo ng'ara kwenye majimbo mengi katika nafasi za Ubunge na Udiwani vimeibuka kuwa washindi ,na matokeo ya nafasi ya Urais yameendelea kutangazwa na leo ndiyo atangazwa mshindi kwa nafasi ya Urais kulingana na uwingi wa majimbo aliyopata ushindi na kujumuisha matoke.Na kuibuka kidedea leo.
Vyama vilivyoingia katika kinyang'anyiro vilivyo shindwa vikubali matokeo,kukataa matokeo bila kufanya utafiti wa kutosha kwa wapiga kura wako,ni kushangaza watu.kushinda au kushindwa ni katokeo ya idadi ya wapiga kura waliyo kukubali au kukukataa.Na si rahisi kung'amua ni nani aliye nikubali au kukukataa kwa kuwa ilikuwa ni siri ya mpiga kura kwenye visanduku.
Lakini pia kushinda au kushndwa kusichukulie uwingi wa watu waliyojitokeza siku mgombea alipokwenda kunadi sera za chama chake,watu wanaweza wakawa wengi lakini siku ya kupiga kura wasiwe wengi au wakawa wengi lakini hawa kuwa na shahada ama walikuwa na shahada hawa kwenda kupiga kura yote yanawezekana kwa Binadamu.
Aidha cha msingi Tume ya Uchaguzi irekebishe utaratibu wa kuchelewesha kutangaza matokeo,ucheleweshwaji wa kutangaza matokeo kuna sababisha maswali mengi kwa wapiga kura wenyewe,wanacha wa vyama mbalimbali na wagombea wenyewe,kwanini yanacheleweshwa.Matokeo yakitangazwa mapema yatapunguza malalamiko ya wapigiwa kura ya kuchakachuliwa kura zake.
No comments:
Post a Comment