Thursday, November 18, 2010

Wabunge wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa baraza la mawaziri watakaoteuliwa hapo baadaye

Rais Kikwete akitia saini baada ya kumwapisha waziri Mkuu Mizengo Pinda Ikulu ya Chamwino Dodoma leo na saa 10.30 alihutubia Bunge,ambapo waheshimiwa wabunge wa CHADEMA walitoka nje ya Bunge hilo mbele yake kwa tishio la kususia hotuba yake.

Pamoja na hayo Rais aliendelea na hotuba yake na Wabunge wa CCM na Vyama vingine ya Upinzani waliokuwemo.Na kuweka kambi isiyo rasmi Bungeni humo

RAIS Jakaya kikwete amewataka wabunge wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,kutoa ushirikiano wa kutosha kwa baraza la mawaziri watakao tuliwa baadaye,ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi wa kutosha.

Dokta Kikwete alisema hayo wakati alipoto hutuba yake ya kufungua Bunge la kumi la Jamhuri ya Mungano wa  Tanzania,mjini Dodoma leo na kutagaza vipaumbele vyake vya kuleta maendeleo vitakavyo tekelezwa ndani ya miaka mitano ijayo.

Alitaja baadhi ya vipaumbele hivyo ni pamoja na kusogeza huduma za afya  kwa kuoboresha huduma zake,na kuongeza bajeti katika sekta ya afya,kuimarisha sekta ya madini,kuboresha miundo mbinu ya barabara, na reli,kuanzisha benki ya kilimo.

Vingine ni pamoja na kuimarisha sekta ya elimu kwa kuboresha mazingira
yakujifunzia na kufundishia na kutoa maslahi kwa walimu kujenga nyumba za walimu,kuimarisha sekta ya utalii ambayo ni ya pili kwa kuiingizia fedha za kigeni nchini.

Nyingine ni kumkomboa mwananchi kwa kuendeleza programu ya kilimo nchini,kwani mazo ya chakula na biashara yameongezeka kweli msimu huu,na kuimarisha sekta ya viwanda kwa kuendeleza viwanda,na kuimarisha sheria mpya ya kupambana na rushwa.

Kipaumbele kingine ni pamoja na kuendeleza vipaji vya wasanii,wa muziki,filamu,maigizo na kuimarisha michezo itakayo fundishwa  shuleni,walimu wenye fani za michezo wafundishe michezo,na kuimarisha utoaji wa haki kwa wananchi.

Pia Dkt Kikwete alisistiza kuwa yeye ni Rais wa wote waliomchagua na wasio mchagua,wakiwa na matatizo watakwenda kwake kusema shida zao,ni Rais aliyechaguliwa na  CCM na vyama vingine.

Aidha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda alitoa shukurani kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa maelekezo ya kutekelezwa baada ya kuteua baraza la mawziri, ambapo akiwa kiongozi mkuu wa serikali atatekeleza kwa kusaidiana na baraza la mawaziri na wabunge wote.

Mhe.Pinda alitoa angalizo kuhusu umoja wa watanzania kuwa usigeuzwe kuwa jambo dogo,wala asiruhusiwe mtu mmoja mmoja,kikundi cha watu au chama kuonyesha dalili ya uvunjifu wa amani nchini.

Alisema kuwa kuna baadhi ya vyama haviwa tii moyo hata kidogo wananchi,kwa hali hiyo si mwelekeo mzuri kwa nchi yenye amani na utulivu Tanzania,na kupongeza ukuzaji wa kipato cha mwananchi kwa kuendeleza sekta ya kilimo,ufugaji na uvuvi.

Alitoa ahadi kuwa ataekeleza magizo hayo kwani kila mbunge amaetoka kwa wananchi wenye vipato vinavyotegemea kilimo na kisha  aliairisha Bunge hilo hadi tarehe 8/2/2011 saa 3.30 asubuhi.

No comments:

Post a Comment