Thursday, November 18, 2010

Dkt Slaa kutomtambua Rais Kikwete kunazua maswali mengi miongoni mwa watanzania

Dkt Slaa  wa CHADEMA katika Hekaheka za kutafuata Urais wa Tanzania 2010 ( Source Christian Sikapundwa)


KUFUATIA kauli ya Dkt Wilbroad Slaa ya kutomtambua Rais wa Jamhuri ya Muungno wa Tanzania Dkt Jakaya Kikwete,kunazua maswali mengi kwa baadhi ya watanzania wenye akili sawasawa, wenye kujua asiyekubali kushindwa si mshindani.

Kwa mujibu wa kauli hiyo wabunge wa chama chake cha CHADEMA nao bila kujua, kwa makusudi, kuwa waliapa mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Anne Makinda kuwa watakuwa waaminifu, watailinda,wataitete katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumalizia kusema Mungu awasaidie.

Lakini cha ajabu haohao waliosema hivyo, kwa kufuata kauli ya Slaa asiyekubali kushindwa na kutomtambua Rais Kikwete,leo wamekataa kushiriki kuapishwa kwa waziri Mkuu wa Jamhuri ya Tanzania Mhe. Mizengo Pinda, katika Viwanja vya Ikulu Chamwino Dodoma.

Zaidi ya hayo wanaendelea kuwa watasusia hotuba ya Mhe.Rais Kikwete, itakayo tolewa leo moja kwa moja na Vyombo vya habari, kufuatia kauli ya Rais wao Dkt Slaa,  aliyeshindwa kuwa Rais halali wa nchi hii, hivyo wanataka  wananchi na jamii ya kimataifa ambayo ilithibitishiwa na watazamaji wa ndani na nje wakiwemo TEMCO, SADC,EAC,EU, UN kuwa uchaguzi ulikuwa huru na wahaki.  CHADEMA wanataka  kujenga Tanzania ya namna gani?.

Wananchi wanaanza kuwa na maswali mengi kufuatia uamuzi wa wabunge hao kati yao ni wasomi, hivyo hao wamesoma vyuo gani ambako hawakujifunza Saikolojia,Lojiki ya mambo yanavyo kwenda katika ulimwengu huu.

Kuchaguliwa au kutochaguliwa ni matakwa ya yule atakaye kukuchagua au kutokuchagua,hivyo hayo hawayajui? au mradi kuuonyesha ulimwengu kuwa wao wanaweza kususia,hivyo ni wote walikubaliana au ni ‘msafala wa mamba na kenge  nao wapo’.

Kama utafanikiwa kusoma Blog hii, jaribu kumrudia Mungu wako na kusema Eee Mungu nisamehe,na urudi Tanzania maana ninyi tunakuwa na mashaka nanyi,mnaelekea kubaya,wale wenzenu wamezoea,wamekulia katika hekeheka za kutengena na familia zao,kwetu ni jambo geni linahitaji maandalizi ya kutosha.

Watanzania hawajui, na hao wafuasi ambao wanawashabikia si lolote,hawana mbinu za kujihami,kutokana na hali zao zilivyo,tusipoteze amani na utulivu tuliouzoea, Baadhi ya nchi duniani zimekubaliana na matokeo uchaguzi 2010 na sheria,kanuni na taratibu zilizotawala uchaguzi huo zilifutwa ikiwa ni pamoja na kandaa uwanja sawa wa ushindani hapakuwa na malalamiko.

Hivyo hao waliosusia kuapishwa Waziri Mkuu Pinda,na baadaye kususia hotuba ya Rais Bungeni hapo baadaye,wataingia tena katika Mjengo wa Bunge? kuendelea na vikao vyake,wenyewe wanajionjaje kwa wenzao? Wabunge wenzao wa chama Tawala CCM na kambi vyingine za upinzani ambao si CHADEMA nao wanawaonaje? Jamii ya watanzania wanawaonaje? bado watakuwa na imani na chama hicho ( CHADEMA )


No comments:

Post a Comment