Monday, November 29, 2010

FEDHA ZA UJENZI WA BARABARA ZITUMIKE KWA UJENZI ULIO BORA WA BARABARA ZETU - DKT ISHENGOMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt Christine Ishengoma katika kikao cha Board ya barabara Songea Club tarehe 26/11/2010

MKUU wa mkoa wa Ruvuma  Dkt Christine Ishengoma amekemea tabia ya baadhi ya Halmashauri mkoani hapa kutumia fedha za ujenzi wa barabara visivyo hasa kujenga vipande virefu bila ubora. ‘Afadhali mjenge barabara km  moja ( 1 ) yenye ubora kuliko km 4 kwa fedha hiyo bila ubora.’Alishauri Dkt Ishengoma.

Baadhi ya wajumbe wa kikao cha Bodi ya barabara mkoani Ruvuma kilichoketi tarehe 26/11/2010 Songea Club walipeleka masikitiko yao makubwa kwa halmashauri ya Manispaa  ya Songea. Kwa ujenzi wa barabara na matengenezo bila viwango.

Hata  hivyo waliipongeza,Halmashauri ya Mbinga katika ujenzi wa barabara za kiwango cha lami pia wakala wa Barabara mkoani TANROADs kusimamia vyema mitandao na kujenga barabara na madaraja.( Source Juma Nyumayo )

No comments:

Post a Comment