Monday, November 29, 2010

Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya akemea vitendeo vya Wizi wa Ruzuku za Pembejeo

'Sikubali wala sinataruhusu Ruzuku za pembejeo zilizotolewa na serikali kuliwa na wajanja wachache wenye lengo la kuchukua vocha za mbolea na mbegu wakati mashamba hawana ili wakauze wapate fedha,sintavumilia kwa vitendo vya kuhujumu fedha za serikali.' Alisisitiza mkuu wa wilaya huyo kwenye kikao cha  maendeleo cha mkoa ( RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Songea club.




Mkuu wa Wilaya ya Songea Bwana Thomas Ole Sabaya ambaye ni mwenye kiti wa Pembejeo za Ruzuku wilaya  ya Songea,ndiye aliyeanzisha utaratibu wa barua za utambulisho wa shamba kwa wakazi wa mjini ili kulinda fedha za Serikali zisiliwe na wajanja wachache ambao hujifanya wana mashamba kumbe wanalengo la kuiba fedha za serikali kupitia Ruzuku za pembejeo,kitendo ambacho kinamkera Mkuu wa wilaya hiyo.

Aidha Bw.Sabaya amekemea kwa nguvu zote vitendo vivyosadikiwa vinafanywa na baadhi ya Watendaji na Wenyeviti wa Mitaa vijijini na Vitongoji kutoza fedha kati  ya shilingi 1,000/= hadi 5,000/= ili kuwapitishia barua hizo kuwa ni kero na ni dalili za rushwa na wakibainika watachukuliwa hatua kali za kinidhamu,(Source Juma Nyumayo)

No comments:

Post a Comment