Saturday, November 27, 2010

WABUNGE WA CHADEMA WALISUSIA HOTUBA YA RAIS KIKWETE BUNGENI KWA KUTORIDHISHWA NA MATOKEO YA KURA ZA URAIS

 Mhe.Freeman Mbowe katika mdahalo wa kambi mbili ndani ya Bunge la 10 linatoa picha gani kwa wapigakura wao uliofanyika Jijini Dar es salaam Jumamosi ( Picha na Christian Sikapundwa }

Kiongozi wa Kambi ya upinzani katika Bunge la 10 Mhe.Freeman Mbowe alisema kutoka katika Bunge wakati Rais kikwete akifungua Bunge la 10 Mjini Dodoma hivi karibuni, wabunge wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema ni kuwakilisha kilio chao mbele ya Rais,Wabunge wa vyama vingine na Chama Tawala pamoja na wanachi kuwa kitendo cha Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Urais  katika baadhi ya majimbo si mzuri.Ufanyiwe marekebisho.

Aidha alisema kuwa wao hawajsema kuwa hawamtambui Rais Kikwete,bali kilio chao ni matokeo ya uchaguzi yalikuwa na kasoro,na alisema wataendelea kushirikiana na wabunge wote ili kuleta mustabali wa kumletea mwananchi maendeleo ambao ni wapiga kura wao.


1 comment:

  1. Tunaweza kuwa na mawazo mbali mbali kuhusu kitendo cha wabunge wa CHADEMA kususia hotuba ya JK. Wako wanaodai kwamba CHADEMA wamekataa kumtambua JK kama rais, kwamba wamekataa kuitambua serikali ya JK. Huu si ukweli.

    Dr. Slaa alielezea wazi wazi msimamo wa CHADEMA. Wao wana ugomvi na mchakato wa kutangazwa matokeo ya kura ya urais. Wanatambua kuwa kwa mujibu wa taratibu zilizopo, JK ni rais. Walisusia hotuba yake kama njia ya kuwasilisha malalamiko yao, baada ya juhudi zao nyingine kugonga mwamba.

    Mimi, raia ambaye si mwanachama wa chama chochote cha siasa, msimamo wangu nimeulezea katika makala hii hapa.

    ReplyDelete