Saturday, November 20, 2010

JIAJIRI KUPITIA UFUNDI PIKIPIKI MWONE JOHN JOHN KOMBA SODECO SONGEA

 Fundi pikipiki Bw.John John Komba akiwa dukani kwake,ukihitajika spare ya pikipiki hakuna haja ya kwenda kununua kwa mwenzake.
Fundi John Komba akimwelekeza mwanafunzi wake wa mwaka wa pili Bw.Emelian Mbepela kufunga taa za pikipiki aina ya SANLG,ni aina za pikipiki zilizoko kipindi hiki,aina ya SUZUKI kwa mwanafunzi kama huyu itakuwa shida kwake.


UFUNDI wa kutengeneza pikipiki Katika Manispaa ya Songea umesaidia sana vijana wengi kujiajiri baada ya kupata mafunzo hayo kwa miaka miwili tu,kisha kwenda kufungua gereji zao mitaani,ndani ya Manispaa au nje ya manispaa hiyo.

Fundi pikipiki katika maeneo ya SODECO katika Manispaa ya Songea Bwana John John Komba alibainsha hayo kwenye gereji yake kuwa alianza kujiunga katika fani hiyo mwaka 1985 na kuhitimu mwaka 1988.

Alisema kuanzia mwaka 1988 aliafungua gereji yake Mahenge katika manispaa hiyo hiyo ambapo alianza kupokea vijana waliotaka kujifunza,kipindi kile kila kijana alilipa sh.50,000 tu lakini mabadiliko ya nyakati,kijana anatakiwa kulipa sh.200,000. Na mafunzo ni kwa miaka mitatu.

Aidha alisema tangu aanze kufundisha vijana hao ni zaidi ya 15 wapitia katika gereji yake,na wamekwisha jiajiri katika wilaya za Mbinga,Tunduru,Namtumbo  na katika Manispaa ya Songea.kwa sasa ana wanafunzi wanne.

Kwa mzamzi yeyote mwenye mtoto anayehitaji kujiajiri kupitia ufundi pikipiki amwone Fundi JJ Komba,zaidi ya hayo ana duka la spare parts za pikipiki SODECO Songea Mkabala na Soko la kuuza mazao ya chakula.

1 comment:

  1. Nimevutiwa na habari hii. Inatia moyo kuona uzalendo wa watu kama Fundi John Komba, wa kuchangia utatuzi wa tatizo la ajira. Hongera, Fundi Komba, na kila la heri.

    ReplyDelete