Friday, November 26, 2010

MHE.DKT.CHRISTINE ISHENGOMA AKERWA NA WAHARIBIFU WA MAZINGIRA MKOANI RUVUMA

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe.Dkt.Christine Ishengoma akiongea na wadau wa maendeleo mkoani wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri wa mkoa ( RCC ) katika ukumbi wa Songea Club naja ( Source Christian Sikapundwa ).

MKUU wa Mkoa wa Rvuma anakerwa na watu wanaochangia uharibifu wa mazingira katika mkowa wa Ruvuma kwa kuchoma mkaa,kukata  miti bila kupanda mingine,kuchoma misitu bila sababu,kitendeo ambacho kitakaribisha ukosefu wa mvua na hatimaye kuwepo kwa jangwa.

Mkuu wa mkoa huo alisema hayo jana wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa (RCC ) katika ukumbi wa Songea Club,ambapo aliwataka wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani hapo kuzingatia kanuni za kuhifadhi mazingira na kuyatunza,na wachoma mkaa wapewe vibali vya kufanya shughuli hizo.

Dkt.Ishengoma alisema utekelezaji wa miradi ya Millenia ( millennium Challenge ) umeanza kuanzaia Jun mwaka huu kwa kuanza na ujenzi wa barabara kwa viwango vya lami.Songea hadi Namtumbo kilometa 67 kwa mkataba wa miezi 27 ambao utaishia September 2012.

Nyingine ni Barabara ya Peramiho hadi Mbinga inayojengwa na kampuni ya Sinohydro Corporation Ltd amekabidhiwa mradi huo mwezi Agasti mwaka huu kwa mkataba wa miezi 27 na atakabidhi mradi huo mwezi Oktoba  mwaka 2012.

Aidha Dkt Ishengoma alisema uchangiaji wa maoni,ushauri wa wajumbe wa kikao hicho kinachangia maendeleo ya Mkoa wa Ruvuma kwa kiwango cha juu,alisema mkoa unaendelea kujitosheleza kwa mazao ya chakula na kuzalisha ziada kwa ajili ya kuuza ndani na Nje ya mkoa.

Alisema wananchi wasiuze mahindi yote bali waache mahindi mengine kwa ajili ya chakula chao na familia zao,alisema uzalishaji umeongezeka kutoka tani 652,462 msimu wa 2008/2009 hadi tani 1,127,589 msimu wa kilimo wa 2009/2010 sawa na asilimia 72.8.

Alisema mkoa umelenga kuzalisha tani 107,882 za mazao ya chakula na tani 1,149,164 za mazao ya biashara na amewapongeza wakulima wote kwa ujumla wao wa mkoa huo kwa kuzalisha mazao ya chakula na biashara ingawa kulikuwa na mapungufu ya kitaalamu yalijitokeza katika kilimo musimu uliyopita.

Pia alisema Serikali imeshatoa shilingi 12,809.000.000/= za kununulia mahindi hadi sasa tani 37,090.4 zenye thamani ya shilingi 11,,410,010,460/= na ununuzi unaendelea,alisema mkoa umepokea Vocha 518,060 za Ruzuku ya pembejeo zenye thamani ya shilingi 10,781,360,000/= zitakazo nufaisha wakulima 172,900 kwa musimu wa kilimo uliyopita.

Katika musimu huu wa kilimo wakulima 203.412 sawa na ongezeko la asilimia 17.9 watanufaika na ruzuku ya pembejeo,ambapo Wizara imetoa Vocha za mbolea ya kupandia 203,412 zenye thamani ya shilingi 5,288,712,000/= na vocha za mbegu 203,412 zenye thamani ya shilingi 4,041,040,000/=

No comments:

Post a Comment