Saturday, November 13, 2010

MKOA WA RUVUMA WAPOTEZA MRATIBU WA KIFUA KIKUU NA UKOMA BWANA RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU KWA TATIZO LA KISUKARI NA MOYO


HISTORIA FUPI YA MAREHEMU RENE JOSEPH LEOPOLD MWIKWA MRATIBU WA KIFUA KIKUKU NA UKOMA HOSPITAL YA MKOA WA RUVUMA ALIYEFARIKI TAREHE 12/11/2010 SAA 9 ALASIRI.

Alizaliwa tarehe 01/3/1952 Kidodi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro,akapata elimu ya msingi Lumango Luhembe kidodi.Hatimaye alipata elimu ya Sekondari nchini Uganda kidato cha kwanza hadi cha tatu,machafuko ya kisiasa yalivyoanza nchini Uganda,Marehemu alirudi Tanzania.

Alivyorudi Tanzania alijiunga na chuo cha waganga wasaidizi ( watabibu ) Wilayani Kilosa mkoa wa Morogoro,baada ya mafunzo hayo alipelekwa kuanza kazi ya ugnaga Wilaya ya Mbinga Mkoa wa Ruvuma mwaka 1976 ambapo alifanya kazi kwa muda mfupi.

Mwaka 1979 alihamishiwa katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma ambapo mwaka 1980 alikwenda kwa masomo ya stashahada  chuo cha uganga Bumbuli  Tanga mwaka 1982 alihitimu mafunzo yake na kurudi hosipitali ya mkoa wa Ruvuma kama Mratibu wa Kifua kikuu na Ukoma hadi mwka 2006.

Mwaka alianza kupata tatizo la kisukari na moyo,ambapo tarehe 26/12/2006 tatizo likazidi kuwa kubwa na akaendelea kuugua hadi tarehe 12/11/2010 saa 9 alasiri Mratibu Mwikwa akafariki katika hospitali ya mkoa ya Songea,Na mazishi yatafanyika tarehe 15/11/2010 Mjimweme katika manispaa ya Songea,ambako  familia yake inaishi hapo.Marehemu ameacha mke na watoto kadhaa.

Atakumbukwa na watu wengi kwa utendaji wake wa kazi ambao haukuwa na mpaka,hakujali umbali wala unyanyapaa wa aina yoyote.Alikuwa mwepesi wa kutoa ushauri na kutoa msaada kwa wagonjwa wake,alikuwa mcheshi,mwingi wa tabasamu,na maneno ya kumtia mgonjwa faraja.Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi.

No comments:

Post a Comment