Sunday, December 12, 2010

KIPINDUPINDU CHA LIPUKA NKUUNGU NA MAJENGO MANISPAA YA DODOMA

 I meripotiwa kuwa wagonjwa 14 wa kipindupindu kulazwa katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa kipindu pindu katika Manispaa ya Dodoma katika maeneo ya Nkuungu na majengo.

Kufuatia mvua zilizonyesha katika maeneo kadhaa mkoani hapo,uchafu na maji machafu na matunda yanayouzwa na kuliwa bila kuyaosha na kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka kujisaidia kumeletea mlipuko huo.

Taadhari limetolewa na uongozi wa mkoa,kuwa wananchi wanashuriwa kuepuka kula vitu vya baridi,kuondoa uchafu kwani kipindupindu kinatoletwa na kula kinyesi kinacho sambazwa na inzi,kila mmoja anashauriwa kunawa mikono kwa sabuni baada ya kutoka chooni.

No comments:

Post a Comment