MKOA wa Ruvuma imefaulisha kwa asilimia 47.98,ya wanafunzi watakaoingia kidato cha kwanza mwaka huu,ikiwa imeshuka kwa asilimia 8.02 kwa matokeo ya mtihani wa taifa uliyofanyika mwaka 2009.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mshauri wa Elimu wa Mkoa wa Ruvuma Bibi Paulina Mkonongo,mbele ya Kaimu katibu Tawala wa Mkoa huo,alisema wanafunzi 30,829 mkiwemo wavulana 14,986 na wasichana 15,843 waliofanya mtihani huo mwaka huu,kati yao 14,792 mkiwemo wavulana 7,537 na wasichana 7,255 ndio walio faulu sawa na asilimia 47.98. Ambao wataingia kidato cha kwanza mwakani.
No comments:
Post a Comment