Hicho ndicho kikosi cha timu ya Wana- Lizombe Majimaji ya mkoani Ruvuma iliyoilaza Polisi ya Iringa 3-2 katika uwanja wao wa nyumbani wa majimaji.
Mgeni rasmi katika mechi hiyo Injinia Steven Shauri akisalimiana na wachezaji wa timu ya majimaji wakati wa kukagua timu.
Hicho ndicho kikosi cha wanausalama Polisi Kutoka Iringa ambao kabla ya mchezo wa leo walikuwa wa pili kutoka City Mbeya ambayo ilikuwa ikishikilia nafasi ya kwanza katika michozo ya Ligi daraja la pili.Ambapo majimaji walikuwa watatu katika msimamo wa ligi,Lakini baada ya kushinda leo Majimaji ipo katika nafasi nzuri.
Injinia Steven Shauri akisalimiana na wachezaji wa timu ya Polisi Iringa katika uwanja wa majimaji leo ambapo wameshindwa kutamba mbele ya wana lizombe hao wa Majimaji. walipochabangwa bao 3 kwa 2.
TIMU
ya soka ya Majimaji imefunga timu ya
Polisi Iringa magoli 3 kwa 2 katika
mechi iliyochezwa katika uwanja wa majimaji mjini Songea leo katika ligi ya
daraja la pili.
Mchezo
ulikuwa wa vuta ni kuvute katika dakika ya 14 Polisi Iringa ilianza kuliona
lango la Majimaji kupitia mchezaji wake Demoso Mbalika jezi namba 11
mgongoni,Lakini katika dakika ya 19 majimaji ilisahwadhisha goli hilo kupitia
mchezaji wake Sixmundi Mwasikaga namba 15.
Mambo
yalikuwa hivyo ambapo katika dakika ya Tito Sanga namba
2 aliipatia timu ya Polisi Iringa
bao la pili alilolifunga katika dakika ya 22 , katika patashika hiyo naye
mchezaji wa majimaji Edward Philipo Songo jezi namba 10 alilisawadhisha bao hilo katika dakika ya 24.
Hadi kipenga kupigwa katika kipindi cha kwanza ilikuwa Majimaji 2 na Polisi
Iringa 2.
Katika
kipindi cha pili timu zote ziliingia uwanjani kwa nia ya kupata ushindi
ukizingatia Polisi Iringa Ilikuwa ya pili katika msimamo wa Ligi ya daraja la
kwanza nyuma ya Mbeya
City inayo ongoza Ligi
hiyo ambapo majimaji walishika nafasi yatatu, kabla ya kushinda mechi ya leo.
Katika
dakika ya 59 kipindi cha pili majimaji ilipata bao la tatu kupitia mchezaji wake Edward Songo,goli ambalo
lililoipaia majimaji ushindi wa magoli 3 – 2 hadi kipenga cha mwisho. Wakati
Pilisi Iringa ilipata kadi 1 na Majimaji kadi 3.
Kutokana
na matokeo hayo yamezidi kuiweka majimaji katika nafasi nzuri katika msimamo wa
ligi hiyo.Maji maji itakuwa na kibarua kingine na timu ya Mkamba kutoka
Kilombero tahere 2/3/2013, tarehe 9/3/2013 na JKT Mlale na tarehe 13/3/2013 na Mbeya City.