Tuesday, September 13, 2011

WANA - BLOG YA TUJIFUNZE KUSINI IPO KATIKA KUUNGANA NA NDUGU,JAMAA WALIYO POTEZA NDUGU NA JAMAA ZAO KATIKA AJALI YA MELI HUKO PEMBA

Blog ya TUJIFUNZE KUSINI ina toa pole kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar kwa kupoteza nguvu kazi yake kutokana na ajali ya meli ambayo imewapa watanzania wakati mgumu wa majonzi. Kama waswahili wasemavyo ) kuwa mtu akiumwa na nyoka ,akiona kamaba anashtuka.Ajali hiyo imewakumbusha Wa - Tanzania ajali ya MV Bukoba ambayo haitasahaulika na watanzania walio wengi.Pole kwa familia zilizokumbwa na matatizo hayo

Lakini kama ni kosa kama lile la MV Bukoba,Serikali ifuatilie maana uzembe wa wachache unasababisha maangamizi ya maisha ya watu,kama meli ina uwezo wa kuchukua abiria 600 sasa iweje ichukue abiria 800 na mizigo,kwa vyovyote ilizidiwa na mzigo na ule mzigo meli haijachue yenyewe ikasema basi bali ni watu wenye akili ya kujua sasa meli imejaa iondoke ,lakini walivaa nafsi zisizojali uhai wa wengine.

No comments:

Post a Comment