Friday, September 23, 2011

UMEYA MANISPAA YA SONGEA NI VITIMBWI TUPU, MAKAMU MEYA ATIMKA NA KURA MADIWANI WA CHADEMA WAMKIMBIZA AIBU TUPU ,MEYA AVUA JOHO

Leo ndiyo leo hao waheshimiwa madiwani ni wa chama TAWALA na wa CHADEMA lakini Madiwani wa CCM ni wengi kuliko wa CHADEMA,cha ajabu madiwani hao katika kupiga kura za kuchagua Mstahiki Meya Mheshimiwa Charles Mhagama,ni kwamba  waliyo sema ndiyo ni 12 na waliyo sema hapana ni 14 hiyo ina maana hata baadhi ya Madiwani wa CCM walikuwa hawana imani na Mheshimiwa Mhagama kuwa Meya wa Manispaa ya Songea.

Kutokana na matukio yaliyotokea leo ya kumtangaza Meya mpya Mhe.Charles Mhagama katika manispaa hiyo kutangazwa na Makamu Meya badala ya Mkurugenzi wa Manispaa,ndipo madiwani wa CHADEMA na CCM kutoridhishwa na matokeo hayo.kesho nitakuletea na baadhi ya picha za vurumai hizo za kuwania Umeya.Hiyo ni dalili mbaya kiuongozi,maana Meya huyo atakuwa katika wakat mgumu kuongoza Manispaa hiyo kwa kutokuwa na imani  naye.


No comments:

Post a Comment