Thursday, September 22, 2011

VIONGOZI WA WANANCHI WA MANISPAA YA SONGEA LEO WAMEMPOKEA MKUU MPYA WA MKOA WA RUVUMA BWANA SAID MWAMBUNGU

 Mkuu wa mkoa mpya wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu alipokuwa akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Morogoro,baada Rais Kikwete kumteua kuwa mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,kutoka kwenye wadhifa wa ukuu wa wilaya ya Morogoro.Leo ameripoti katika mkoa wa Ruvuma kwa wadhifa wa ukuu wa Mkoa ( Source MICHUZI )
a
 Waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Songea ni miongoni mwa viongozi waliyempokea mkuu huyo wa mkoa kwa shangwe na furaha,kama ilivyo desturi ya wananchi wa mkoa huo wanavyo jua kupokea watu.
Mhe. Mwambungu anakaribishwa mkoani Ruvuma badala ya Mhe.Dkt Christine Ishengoma aliyehamishiwa mkoa wa Iringa.Mwambungu atapokea changamoto kadhaa katika mkoa huo zikiwemo za umeme,miundo mbinu ya barabara hasa katika manispaa ya Songea,Soko kuu,halina sakafu ,stendi ya mabasi siyo ya kuridhisha.kazi ni kwake .karibu sana Ruvuma ushirikiano na watu aliyowakuta ndiyo kutaleta maendeleo ya mkoa huo.

No comments:

Post a Comment