Friday, September 16, 2011

SOKO LA SIDO MWANJLWA MKOANI MBEYA LATEKETEA KWA MOTO MALI NYINGI ZA WATU ZIMEANGAMIA

 Moto mwingine wa teketeza sokola SIDO lililoko Mwanjelwa Jijini Mbeya uliyo anza takribani saa 3.00 asubuhi ,pamoja na jitihada ya magari ya zimamoto Jijini humi lakini haikuzaa matunda.moto uliwaka utadhani wamemwagia petrol.
 Kama unavyoona hali ilivyo kuwa ,ilikuwa siku ya maswali mengi kwa wana mbeya kwanini masoko ya Jijini humo yanateketea kwa moto? lilianza la Mwanjelwa,likaja la Mbeya mjini,kisha la Tunduma na sasa la SIDO ambalo lilikuwa uti wa mgongo wa mapato ya Jiji hili vitega uchumi vya watu.
a
 Lakini watu nao hasa vibaka walipata vya kupata badala ya kuokoa kwa ajili ya wenye mali bali ni kwa manufaa yao wamepata mitaji bila jasho.
 Ndipo FFU walipo tumia mabomu ya machozi kutawanya wimbi la vibaka hao,hali ilikuwa tete sana hasa kwa wenye maduka ambayo yaliteketea hakuna kilicho okolewa.ikumbukwe wawekezaji hao walikopa kwa lengo la kulipa baada ya kuuza bidhaa hizo lakini bidhaa hizo zote zimekuwa majivu je watalipa lipa vipi?
 Blog hii imekuletea uone tu hali ilivyo kuwa moto ulivyo kasirika katika kuangamiza mali za watu wasio na hatia jijini humo,hata kama haukuwa karibu kushuhudia nini kilicho tokea kwa akina mwanafyale hao umejionea hali ya kutisha ilivyo kuwa,moto ni mzuri kwa kupikia na ukitumiwa vizuri lakini ukitumika bila utaratibu ,moto ni adui mkubwa wa maisha ya watu.
Poleni sana wana - Mbeya Pole Pia Mheshimiwa Kandoro mkuu wa Mkoa anaye kwenda mkoani humo anakaribishwa kwa matukio ya moto,lakini usijali cha msingi utafiti kwa nini masoko jijini humo yanaungua kila mwaka?.

No comments:

Post a Comment