Friday, September 30, 2011

MVUA ZA VULI ZA RASHARASHA ZIMEANZA MJINI MOROGORO

 Mkoa wa Morogoro katika miaka ya 70 ulikuwa na mvua nyingi na ulikuwa ni miongoni mwa mikoa inayozalisha chakula wa wingi.lakini kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na uharibifu wa mazingira,hasa kukata mitikatika vyanzo ya maji,kuchoma mkaa,kuchoma moto misitu,kumesababisha mkoa huo upoteze ratiba zake za mvua kunyesha,hivyo hata namna ya uandaaji wa mashamba unawachanganya waulima wa mkoa huo.

Vyanzo vikuu ni milima ya Uruguru ( Uruguru Mountain ),na milima mingine ya mwambao ya mto Ruwaha,milima hiyo miaka ya nyuma ilikuwa ikibubujisha maji kipindi chote cha mwaka,Ila kwa sasa hali hiyo haipo  kutokana uharibifu wa mazingira atika uchezea uoto wa asili,na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mvua hizi zilianzia Kijiji cha Doma ,Melela ,Morogoro mjini,hadi Mikese.

No comments:

Post a Comment