Monday, September 26, 2011

Chuo Kikuu Songea cha anza,mkuu wachua atambulishwa

 Profesa Donatus Komba akisalimia waumini baada ya kutangazwa kuwa mkuu wa chuo kikuu cha Songea  na Asofu Mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega katika Kanisa kuu la Mtakatifu Mathias Mulemba Kalemba Jumapili iliyopita kwenye ibada ya misia ya kwanza.
 Dokta Kiremire Araka akisalimia waumini baada ya kutangazwa kuwa ndiyo atashirikiana na Priofesa Kapinga katika kupoea wanachuo 250 watakao anza mwezi ujao tarehe 25 katika chuo hicho kipya Kusini mwa - Tanzania
 Askofu Mkuu Norbert Mtega akiwatangaza rasmi Mkuu wa chuo cha Songea cha Sayansi ya Jamii Profesa Donatus Komba na mwenzake Dkt.Kiremie Araka baada ya Ibada ya Misaa takatifu Jumapili iliyo pita.
 Kabla ya kuwatangaza Asofu aliwashika waumini mono wa heri na baraka katika kuchangia mfuo wa jimbo.
 Hapo amekaa wenye kiti chake akisubiri waumini kwende imshika mkono
i
 Profesa Komba wa kushoto mwenye kaunda suti miono mifupi na Dokta Araka  kulia wakitokea eneo walilotambulishwa.
 Hayo ni baadhi ya majengo ya chuo kikuu hicho cha Songea Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Kanda ya kusini.
Baadhi ya waumini waliyo shiriki Ibada hiyo iliyoandamana na michango mbalimbali kutoka katika Parokia za jimbo hilo ambapo parokia ya Bomba mbili na Parokia ya mjini zimetoa Tshs.1,500,000 kila parokia,kisha kuwatangaza Profesa Kapinga na Dokta Araka.


CHUO kikuu cha Songea Kitivo cha Elimu ( Sayansi ya Jamii ) kinatachukua wanachuo 250 kuanzia trehe 25 October mwaka huu kilicho anzishwa na Baraza la Maasofu Tanzania,na mkuu wa chuo hicho katangazwa rasmi na Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Songea Mhashamu Norbert Mtega baada ya ibada yamisa jumapili iliyopita.

Mhashamu Mtega alimtangaza mkuu wa chuo hicho kuwa ni Profesa Donatus  Komba na Dokta Kiremire Araka ambao wataanza kuwapokea wanachuo hao mwezi ujao.

Aidha Asofu Mtega alisema Mkuu huyo wa chuo hicho na mwenzake wakishirikiana na uongozi wa kanisa wataanzisha ( Marafiki wa Chuo kikuu cha Songea ) ‘Songea University Friends’ chenye lengo la kukisaidia chuo hicho.

Kikundi hicho kimeanzishwa tokea Jumapili iliyo pita,alisema wale ambao walikuwa tayari waliambiwa waende wamwone Profesa Kapinga ili waweze ujiandikisha.’ Mwenye simenti,maplastic, fedha wanaombwa kujitolea  au kutoa msaada ili chuo hicho kitimize  malengo yake kusini mwa Tanzania katika Jubilei ya miaka 50 ya Uhuru.

Askofu Mkuu Norbert Mtega pia amewatangazia wananchi wa Manispaa ya Songea ambao wana nyuma kuzipangisha nyumba hizo kwa walimu na watumishi wa chuo hicho na wanafunzi watakao jiunga chuoni hapo kwa kuwa chuo hakina mabweni ya kutosha.

2 comments:

  1. Shukrani kwa taarifa hii murua. Sahihisho kidogo tu ni kuwa jina la mkuu ni Profesa Donatus Komba.

    ReplyDelete
  2. Asant Profesa kwa kusahihisha nakushukuru sana Tuko pamoja.

    ReplyDelete